“Miaka 6, anajilipia ada mwenyewe” – Habiba Zumo

October 12, 2020

Anko Zumo, Habiba Zumo na Mai Zumo ni familia ambayo kuanzia baba, mama na mtoto wote wanafanya kazi moja ya uchekeshaji ambapo wamepata umaarufu mkubwa hapa nchini Tanzanoa na kuingiza pesa.

Sasa mama wa familia hiyo Habiba Zumo amesema kwa sasa mtoto wao Mai Zumo mwenye miaka 6 ambaye yupo darasa la kwanza anaweza kujilipia ada mwenyewe kutokana na kazi anayoifanya.

“Mai Zumo amefanana na bibi yake wa upande wa baba yake, lakini kwa asiyemjua hudhani amefanana na mimi sasa hivi yupo darasa la kwanza ana miaka sita, anaingiza pesa kwa kiasi ambacho yeye anafanya kazi hasa kwa faida yake na maisha yake, sasa hivi anajilipia mwenyewe ada” amesema Mama Mai Zumo.

Aidha baba wa mtoto huyo Anko Zumo amesema moja ya changamoto wanayoipata kutoka kwa mtoto wao kuwa maarufu ni pale wanapopita njiani watu kumshangaa na kutaka kupiga naye picha

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *