Mgombea udiwani Deogratius Ndege azinda kampeni kwa kishindo,

October 6, 2020

Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea udiwani wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Bumera Jimbo la Tarime vijijini,Deogratius Ndege amezindua kampeni za uchaguzi kwa kishindo.

Mgombea huyo ambae anatetea kiti chake alitumia nafsi hiyo kuwaeleza wapiga kura kile alichofanya nadani ya miaka mitano waliomwamini na kumpa kura kuwa ametekeleza miradi kwa shilingi Bilioni 1.1 na kuwa wapiga kura wakimwamini tena kwa kumuunga mkono na kumuongeza miaka  mingine mitano ataenda kukamilisha  miradi iliyobakia.

Ndege aliomba wapiga kura kumwamini na kumpa kura zote za ndio ili kuwa diwani na kura zingine wampe mgombea wa Chama chake John Pombe Magufuli katika nafasi ya urais na mgombea ubunge Mwita Mwikwabe Waitara ili kushirikiana na kuwaletea maendeleo ndani ya halmashauri yake.

katika uzinduzi huo katibu wa Chama Cha mapinduzi wilaya Tarime,Khamis Mkaruka aliwataka watu wa kata ya Bumera kutofanya kosa na wawachague wagombea wa Chama chake ili kuwa viongozi na kuwatumikia na kuwa Rais ameonyesha mfano wa kuingwa katika kutekeleza maendeleo.

Mkaruka aliongeza kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 CCM imejipanga na kuwa itashinda majimbo yote mawili kwa maana ya jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini linalo ongozwa na John Heche wa Chama cha Demkorasia na maendeleo (CHADEMA)

Naye Mbunge wa jimbo la Rorya,Lameck Airo maarufu (LAKAIRO)anayemaliza mda wake aliwataka watu wa Bumera kumchagua Deogratius Ndege na kuwa diwani wakishirikiana na Rais katika kuwaletea maendeleo.

Lakairo alitumia nafasi hiyo kukemea wizi wa mifugo unaotokea mara kwa mara huku akiwataka vijana kuacha tabia hiyo na badala yake wajifunze kufanyabiashara iliyohalali

Lakairo alimaliza kwa kusema kuwa tangu kukua kwake hajawahi kuona mwizi wa mifugo anatajirika badala yake wanajipatia laana na kushindwa kimaisha ambapo aliwataka vijana baada ya uchaguzi kuisha waunde vikundi kwaajili ya serikali kuwapa mikopo na kupata mitaji ya biashara.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *