Mgombea Ubunge wa CUF ahaidi kuwasaidia wakulima, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 1:00 pm

September 1, 2020

      Na Hamisi Nasri,Masasi      MGOMBEA ubunge wa jimbo la Masasi mjini kwa Chama cha wananchi (CUF) Hamza Machuma amesema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha panakuwepo na mkataba wa kisheria kati ya mkulima wa zao la korosho na mununuzi wa zao hilo lengo likiwa ni kulinda maslahi ya wakulima hatimaye waweze kuondokana na adha ya kila mwaka kwa baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao.   Aidha,ameahidi kuwapatia bule vifaa vya kujifungulia akinamama wajawazito katika kata zote 14 za zilizopo katika jimbo hilo la Masasi mjini.   Machuma aliyesema hayo jana mjini Masasi alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo hilo katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha wananchi(CUF) ngazi ya wilaya ya Masasi uliofanyika katika kata ya Mumbaka katika kitongoji cha Mpota mjini Masasi,ambapo Machuma pia alitumia fursa hiyo kuwanadi wagombea udiwani wa kata zaote 14 za jimbo hilo pamoja na wabunge wa jimbo la Ndanda na Lulindi.    Alisema jambo la kwanza ambalo ataanza kulitekeleza iwapo wananchi hao watamchagua kuwa mbunge wao ni kuona wakulima wa zao la korosho waliopo katika jimbo hilo wanakuwa na mkataba maalumu kati yao na mununuzi anayenunua mazao yao ili kuondoa kero ya wakulima kutolipwa fedha zao kama ilivyozoeleka hivi sasa.   Machuma alisema kwa sasa mkulima wa zao la korosho amendelea kunyanyasika kupitia mazao yake ambako amekuwa hana uhakikia wa kulipwa fedha zake pale anapouza korosho zake lakini kwa kuwepo kwa mkataba kama huo utamsaidia mkulima kulipwa fedha zake kwa wakati.     “Ili kuondoa adha ile ya wakulima kutolipwa au kucheleweshewa kulipwa fedha zao za korosho mimi nikiiingia bungeni nitahakikisha  tunaishawishi serikali kuwepo na mkataba kati ya mkulima na mnunuzi kuhusu kulipa fedha kwa wakati hii itamsaidia mkulima kupata fedha zake kwa wakati,”alisema Machuma    Alisema kwa utaratibu uliopo hivi sasa unasema mkulima anapouza korosho zake anapaswa kulipwa fedha zake ndani ya siku saba kama uhalisia haupo hivyo mkulima hukaa muda usioeleweka bila ya kulipwa fedha zake hivyo kukiwepo na mkataba wa kisheria kati ya mkulima na mnunuzi uchewesheji kama huo wa malipo utakuwa ndoto.    Aidha,Machuma alisema kipaumbele kingine ambacho pia atakifanyia kazi ni changamoto ya akinamama wajawazito kukosa vifaa vya kujifungulia wakati wakiwa wodini na kwamba iwapo atakuwa mbunge wa jimbo hilo vifaa hivyo atavitoa bule na kugawa katika kila kata ili kila mama mjazamzito aweze kuchukua na kwenda kuvitumia.   Alisema kipaumbele chake kingine ni kuboresha mifumo ya elimu, upatikanaji wa huduma ya maji hasa maeneo ya pembezoni mwa mji ambako kunaonekana bado kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa huduma ya maji, uboreshaji wa barabara za mitaa pamoja na kupambania upatikanaji wa umeme vijijini (REA) ambapo bado baadhi ya vijiji havijapata umeme mpaka sasa.     Kwa upande wake,kaimu mwenyekiti wa CUF wilaya ya Masasi,Mkomo Katini aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi oktoba 28 kupira kwa wingi na kuchagua wagombea wa CUF kuanzia ngazi ya madiwani, wabunge na raisi ambaye ni Dk.Prof. Ibrahim Lipumba kwani kwa kufanya hivyo kunakuwa na mabadiliko hasa ya kiuchumi kwa wananchi.,

      Na Hamisi Nasri,Masasi  

    MGOMBEA ubunge wa jimbo la Masasi mjini kwa Chama cha wananchi (CUF) Hamza Machuma amesema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha panakuwepo na mkataba wa kisheria kati ya mkulima wa zao la korosho na mununuzi wa zao hilo lengo likiwa ni kulinda maslahi ya wakulima hatimaye waweze kuondokana na adha ya kila mwaka kwa baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao.

   Aidha,ameahidi kuwapatia bule vifaa vya kujifungulia akinamama wajawazito katika kata zote 14 za zilizopo katika jimbo hilo la Masasi mjini.

   Machuma aliyesema hayo jana mjini Masasi alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo hilo katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha wananchi(CUF) ngazi ya wilaya ya Masasi uliofanyika katika kata ya Mumbaka katika kitongoji cha Mpota mjini Masasi,ambapo Machuma pia alitumia fursa hiyo kuwanadi wagombea udiwani wa kata zaote 14 za jimbo hilo pamoja na wabunge wa jimbo la Ndanda na Lulindi. 

   Alisema jambo la kwanza ambalo ataanza kulitekeleza iwapo wananchi hao watamchagua kuwa mbunge wao ni kuona wakulima wa zao la korosho waliopo katika jimbo hilo wanakuwa na mkataba maalumu kati yao na mununuzi anayenunua mazao yao ili kuondoa kero ya wakulima kutolipwa fedha zao kama ilivyozoeleka hivi sasa.

   Machuma alisema kwa sasa mkulima wa zao la korosho amendelea kunyanyasika kupitia mazao yake ambako amekuwa hana uhakikia wa kulipwa fedha zake pale anapouza korosho zake lakini kwa kuwepo kwa mkataba kama huo utamsaidia mkulima kulipwa fedha zake kwa wakati.

     “Ili kuondoa adha ile ya wakulima kutolipwa au kucheleweshewa kulipwa fedha zao za korosho mimi nikiiingia bungeni nitahakikisha  tunaishawishi serikali kuwepo na mkataba kati ya mkulima na mnunuzi kuhusu kulipa fedha kwa wakati hii itamsaidia mkulima kupata fedha zake kwa wakati,”alisema Machuma 

   Alisema kwa utaratibu uliopo hivi sasa unasema mkulima anapouza korosho zake anapaswa kulipwa fedha zake ndani ya siku saba kama uhalisia haupo hivyo mkulima hukaa muda usioeleweka bila ya kulipwa fedha zake hivyo kukiwepo na mkataba wa kisheria kati ya mkulima na mnunuzi uchewesheji kama huo wa malipo utakuwa ndoto.

    Aidha,Machuma alisema kipaumbele kingine ambacho pia atakifanyia kazi ni changamoto ya akinamama wajawazito kukosa vifaa vya kujifungulia wakati wakiwa wodini na kwamba iwapo atakuwa mbunge wa jimbo hilo vifaa hivyo atavitoa bule na kugawa katika kila kata ili kila mama mjazamzito aweze kuchukua na kwenda kuvitumia.

   Alisema kipaumbele chake kingine ni kuboresha mifumo ya elimu, upatikanaji wa huduma ya maji hasa maeneo ya pembezoni mwa mji ambako kunaonekana bado kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa huduma ya maji, uboreshaji wa barabara za mitaa pamoja na kupambania upatikanaji wa umeme vijijini (REA) ambapo bado baadhi ya vijiji havijapata umeme mpaka sasa.

     Kwa upande wake,kaimu mwenyekiti wa CUF wilaya ya Masasi,Mkomo Katini aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi oktoba 28 kupira kwa wingi na kuchagua wagombea wa CUF kuanzia ngazi ya madiwani, wabunge na raisi ambaye ni Dk.Prof. Ibrahim Lipumba kwani kwa kufanya hivyo kunakuwa na mabadiliko hasa ya kiuchumi kwa wananchi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *