Mgombea Ubunge Nanyumbu ahaidi kuwajengea madereva bodaboda ofisi ya kisasa, on September 12, 2020 at 1:00 pm

September 12, 2020

Na Hamisi Nasri, Nanyumbu    MGOMBEA ubunge jimbo la Nanyumbu kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Mhata Yahya ametoa ahadi ya kuwajengea ofisi ya kisasa na yenye ubora waendesha bodaboda wa wilaya hiyo ili waweze kufanya shughuli zao kwa utaratibu mzuri na wenye. malengo ya kuinua uchumi wao.   Yahya alisema hayo jana wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi wa jimbo hilo katika sherehe za uzinduzi wa kampeni zake za kugomgea ubunge katika jimbo hilo la Nanyumbu, uzinduzi huo katika kata ya Chipuputa, kijiji cha Chipuputa.    Alisema iwapo wananchi wa jimbo hilo watamchagua na kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo amejipanga kufanya mambo mengi makubwa ya kimaendelea ili kuwafanya wananchi hao waweze kusonga mbele kiuchumi, kijamii na kisiasa.   Yahaya alisema yeye amejipanga na vipaumbele vyenye tija kwa ajili ya wananchi wa jimbo hilo moja ya kipaumbele ni pamoja na kuwajengea waendesha bodaboda ofisi ya bora ya kisasa ambayo wataitumia kwa kuratibu shughuli zao kwa utaratibu mzuri.   Alisema pia waendesha bodaboda hao watapatiwa mikopo ya aina mbalimbali ya kiuchumi kwa ajili ya kuendesha shughuli za ujasiliamali ambazo kupitia ofisi hiyo atakayeijenga mbunge itawasaidia kuweza kuratibu mambo yao kwa ufanisi zaidi.    Alisema kwa sasa kundi hilo la bodaboda linafanya shughuli zake bila ya kuwa na ofisi maalumu na hiyo inachagia kushindwa kukuza uchumi wao lakini wakipata ofisi yao wanaweza kubuni mambo mbalimbali ya kiuchumi ya kufanya wakiwa katika ofisi yao.  “Bodaboda nitawajengea ofisi mzuri kubwa ambayo haijawi kujengwa katika ukanda huu wa kusini lengo nione kundi hili wanafanya kazi zao katika utaratibu mzuri kama ilivyo makundi mengine pia nitawapa mikopo ya ujasiliamali ambapo hiyoo inaulazima wawe na ofisi,”alisema Yahya.    Yahya alisema kuwa kipaumbele kingine atakachokifanya ni kuhakikisha mradi wa maji kutoka Mto Ruvuma mpaka Mangaka unakamilika na kutoa maji kwa wananchi wa jimbo wa hilo,mradi huo ambao tayari serikali imeshatoa fedha zake za kuanza utekelezaji wake hivyo atasimamia kama mbunge ili uweze kutekelezwa kwa ufanisi na kuendana na thamani ya fedha.    Alisema kundi la wanawake pia atalipakipaumbele kwa kuwapatia miradi mbalimbali ya kiuchumi ili aweze kuanzisha shughuli za kimaendeleo zitakazoweza kuwaletea maendeleo ndani ya familia zao kwani kundi hilo kwa muda mrefu limekuwa likikosa fursa ya kuangaliwa na kusaidiwa.   Naye mwenyekiti wa CCM mkoa,Yusuf Nannila alisema wananchi wa jimbo la Nanyumbu waichaguwe CCM kupitia mafiga yake matatu ambayo ni mgombea uraisi,Dk.John Pombe Magufuli, mbunge wa Nanyumbu , Mhata Yahya pamoja na madiwani wa CCM.    Alisema wananchi hao wanakila sababu ya kuichagua CCM kwa sababu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita serikali yake imetekeleza jumla ya miradi ya yenye zaidi ya thamni ya sh. 40 bilioni hivyo ikipewa ridhaa tena ya miaka mitano itafanya mambo makubwa zaidi ya hayo.,

Na Hamisi Nasri, Nanyumbu  

  MGOMBEA ubunge jimbo la Nanyumbu kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Mhata Yahya ametoa ahadi ya kuwajengea ofisi ya kisasa na yenye ubora waendesha bodaboda wa wilaya hiyo ili waweze kufanya shughuli zao kwa utaratibu mzuri na wenye. malengo ya kuinua uchumi wao.

   Yahya alisema hayo jana wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi wa jimbo hilo katika sherehe za uzinduzi wa kampeni zake za kugomgea ubunge katika jimbo hilo la Nanyumbu, uzinduzi huo katika kata ya Chipuputa, kijiji cha Chipuputa.

    Alisema iwapo wananchi wa jimbo hilo watamchagua na kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo amejipanga kufanya mambo mengi makubwa ya kimaendelea ili kuwafanya wananchi hao waweze kusonga mbele kiuchumi, kijamii na kisiasa.

   Yahaya alisema yeye amejipanga na vipaumbele vyenye tija kwa ajili ya wananchi wa jimbo hilo moja ya kipaumbele ni pamoja na kuwajengea waendesha bodaboda ofisi ya bora ya kisasa ambayo wataitumia kwa kuratibu shughuli zao kwa utaratibu mzuri.

   Alisema pia waendesha bodaboda hao watapatiwa mikopo ya aina mbalimbali ya kiuchumi kwa ajili ya kuendesha shughuli za ujasiliamali ambazo kupitia ofisi hiyo atakayeijenga mbunge itawasaidia kuweza kuratibu mambo yao kwa ufanisi zaidi.

    Alisema kwa sasa kundi hilo la bodaboda linafanya shughuli zake bila ya kuwa na ofisi maalumu na hiyo inachagia kushindwa kukuza uchumi wao lakini wakipata ofisi yao wanaweza kubuni mambo mbalimbali ya kiuchumi ya kufanya wakiwa katika ofisi yao.

  “Bodaboda nitawajengea ofisi mzuri kubwa ambayo haijawi kujengwa katika ukanda huu wa kusini lengo nione kundi hili wanafanya kazi zao katika utaratibu mzuri kama ilivyo makundi mengine pia nitawapa mikopo ya ujasiliamali ambapo hiyoo inaulazima wawe na ofisi,”alisema Yahya. 

   Yahya alisema kuwa kipaumbele kingine atakachokifanya ni kuhakikisha mradi wa maji kutoka Mto Ruvuma mpaka Mangaka unakamilika na kutoa maji kwa wananchi wa jimbo wa hilo,mradi huo ambao tayari serikali imeshatoa fedha zake za kuanza utekelezaji wake hivyo atasimamia kama mbunge ili uweze kutekelezwa kwa ufanisi na kuendana na thamani ya fedha.

    Alisema kundi la wanawake pia atalipakipaumbele kwa kuwapatia miradi mbalimbali ya kiuchumi ili aweze kuanzisha shughuli za kimaendeleo zitakazoweza kuwaletea maendeleo ndani ya familia zao kwani kundi hilo kwa muda mrefu limekuwa likikosa fursa ya kuangaliwa na kusaidiwa.

   Naye mwenyekiti wa CCM mkoa,Yusuf Nannila alisema wananchi wa jimbo la Nanyumbu waichaguwe CCM kupitia mafiga yake matatu ambayo ni mgombea uraisi,Dk.John Pombe Magufuli, mbunge wa Nanyumbu , Mhata Yahya pamoja na madiwani wa CCM.

    Alisema wananchi hao wanakila sababu ya kuichagua CCM kwa sababu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita serikali yake imetekeleza jumla ya miradi ya yenye zaidi ya thamni ya sh. 40 bilioni hivyo ikipewa ridhaa tena ya miaka mitano itafanya mambo makubwa zaidi ya hayo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *