Mfanyabiashara ainunua benki iliyomnyima mkopo,

October 7, 2020

Mfanyabiashara tajiri Adam Deering (39) amepewa jina la Baba wa Motivational Speakers baada ya kusaka pesa kwa nguvu na kuamua kuinunua Benki ambayo ilimnyima mkopo wakati akipambania maisha miaka 18 iliyopita na sasa anawainua Vijana kwa kuwaambiwa wasikate tamaa akijitolea mfano yeye.

“Mwaka 2002 Meneja wa RBS Bank tawi hili la Urmston, Manchester alininyima mkopo akidai sina vigezo vya kupewa pesa, alikuwa Mdada akaniambia Mimi ni mdogo, mtaji wangu mdogo hawawezi kuitoa muhanga pesa yao kwangu, leo nimeamua kuinunua Benki hii na najiona sikukosea kujiamini kuwa naweza bila kuchoka”-Adam

“Niliponyimwa mkopo wa Euro 10,000 niliteseka baadaye nikapambana na nikafungua kiofisi kidogo cha kuweka na kukopa, ofisi haikuwa na kiti wala meza, sikuweza kulipia kodi wala bili, kuna wakati nilijiona kabisa nashindwa ila sikukata tamaa”-Adam

“Nitalikarabati upya hili jengo nimetenga Euro 500,000 na nitaligeuza kuwa Appartment 8 za kufanya biashara ya fedha, kutakuwa na Benki, Taasisi ya mikopo na pia ofisi ya kubadilishia fedha, niwaambie tu Vijana wasichoke kupambana”-Adam

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *