Mfahamu mwigizaji wa nchini marekani Leonardo Dicaprio, on September 17, 2020 at 7:30 pm

September 17, 2020

 Novemba 11, 1974 alizaliwa mwigizaji, prodyuza na mwanamazingira wa nchini Marekani Leonardo DiCaprio.Ametunukiwa tuzo mbalimbali zikiwamo tatu za Golden Globe. DiCaprio alizaliwa jijini Los Angeles akiwa ni mtoto pekee wa Irmelin ambaye alikuwa katibu wa sheria na baba yake George DiCaprio ambaye alikuwa mwandishi, mchapishaji na msambazaji wa vitabu vya vikaragosi. Baba yake ni wa uzao kutoka Italia na Ujerumani. Katika mojawapo ya mahojiano DiCaprio aliwahi kusema yeye ni nusu raia wa Russia kutokana na mababu zake wawili waliopita walitokea nchini Russia.Wazazi wake walikutana Los Angeles walipokuwa masomoni. DiCaprio alipewa jina la Leonardo kwasababu wakati akikaribia kujifungua mama yake alikuwa akingalia michoro ya mchoraji maarufu duniani Leonardo da Vinci katika makumbusho ya Ufizi mjini Florence nchini Italia.Nyota huyo mwaka huu amekusanya kiasi cha dola za kimarekani bilioni 7.2 katika mauzo ya filamu. Mapato hayo yamemweka katika nafasi ya nane ya waigizaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha wa zama zote.DiCaprio ameonekana katika filamu nyingi ikiwamo ya This Boy’s Life. Mwaka huu wa 2019 ameonekana katika filamu ya Once Upon a Time in Hollywood. Mnamo mwaka 2016 alitajwa na jarida la TIME kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi duniani.,

 

Novemba 11, 1974 alizaliwa mwigizaji, prodyuza na mwanamazingira wa nchini Marekani Leonardo DiCaprio.

Ametunukiwa tuzo mbalimbali zikiwamo tatu za Golden Globe. DiCaprio alizaliwa jijini Los Angeles akiwa ni mtoto pekee wa Irmelin ambaye alikuwa katibu wa sheria na baba yake George DiCaprio ambaye alikuwa mwandishi, mchapishaji na msambazaji wa vitabu vya vikaragosi. Baba yake ni wa uzao kutoka Italia na Ujerumani. Katika mojawapo ya mahojiano DiCaprio aliwahi kusema yeye ni nusu raia wa Russia kutokana na mababu zake wawili waliopita walitokea nchini Russia.

Wazazi wake walikutana Los Angeles walipokuwa masomoni. DiCaprio alipewa jina la Leonardo kwasababu wakati akikaribia kujifungua mama yake alikuwa akingalia michoro ya mchoraji maarufu duniani Leonardo da Vinci katika makumbusho ya Ufizi mjini Florence nchini Italia.

Nyota huyo mwaka huu amekusanya kiasi cha dola za kimarekani bilioni 7.2 katika mauzo ya filamu. Mapato hayo yamemweka katika nafasi ya nane ya waigizaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha wa zama zote.

DiCaprio ameonekana katika filamu nyingi ikiwamo ya This Boy’s Life. Mwaka huu wa 2019 ameonekana katika filamu ya Once Upon a Time in Hollywood. Mnamo mwaka 2016 alitajwa na jarida la TIME kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi duniani.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *