Mfahamu mwanamziki Bruno Mars kiundani zaidi, on September 17, 2020 at 7:30 pm

September 17, 2020

 Oktoba 8, 1985 alizaliwa mwanamuziki wa Marekani, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo Bruno Mars. Amekuwa akijulikana kutokana na umahiri wake anapokuwa jukwaani katika staili za Pop, R&B, Funk, soul, Reggae, Hip Hop na Rock. Mara kadhaa amekuwa akisimama na bendi yake inayofahamika kwa jina la The Hooligans.Bendi yake hiyo imekuwa ikitumia vyombo mbalimbali vya muziki, waimbaji na dancers. Jina lake halisi ni Peter Gene Hernandez. Alizaliwa Honolulu, Hawii kwa wazazi Peter Hernandez na Bernadette San Pedro Bayot. Bruno Mars alikulia katika mji wa Waikiki ulio karibu na Honolulu.Baba yake alikuwa ni wa uzazi wa Puerto Rico na Uyahudi wa Ashkenazi kutoka katika nchi za Ukraine na Hungaria. Mama yake alihamia Hawaii akiwa mtoto akitokea Ufilipino na asili kidogo ya uzao wao ni wa Kihispaniola. Wazazi wake walikuwa wanamuziki. Akiwa na ni miaka miwili baba yake alimpatia la Bruno kutokana na mwanamieleka wakati huo aliyekuwa akiwika Bruno Sammartino.Mnamo mwaka 2003 Bruno Mars alienda zake Los Angeles  akiwa na dhamira ya kuinua kipaji chake cha muziki. Akiwa hapo alisaini kuwa na Motown Records ambao baadaye alishindwana kasha Mars akasaini mkataba na Atlantic Records mwaka 2009. Mwaka huo huo alikutana na maprodyuza wakali waliofahamika kwa jina la The Smeezingtons ambao walimfanya Bruno Mars aweze kung’ara.Bruno Mars aliionekana mnamo mwaka 2010 katika “Nothin’ on You” –B.o.B pia track ya Billionaire chini ya Travie McCoy. Hadi sasa Mars ameuza singles zaidi ya milioni 200 na albamu milioni 26 duniani kote hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa best selling artists wa zama zote.Mnamo mwaka 2011 Mars alionekana katika jarida la TIME kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani. Pia Jarida la Forbes ameonekana katika 100 bora za wasanii kwa miaka tofauti tofauti kuanzia 2013.,

 

Oktoba 8, 1985 alizaliwa mwanamuziki wa Marekani, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo Bruno Mars. Amekuwa akijulikana kutokana na umahiri wake anapokuwa jukwaani katika staili za Pop, R&B, Funk, soul, Reggae, Hip Hop na Rock. Mara kadhaa amekuwa akisimama na bendi yake inayofahamika kwa jina la The Hooligans.

Bendi yake hiyo imekuwa ikitumia vyombo mbalimbali vya muziki, waimbaji na dancers. Jina lake halisi ni Peter Gene Hernandez. Alizaliwa Honolulu, Hawii kwa wazazi Peter Hernandez na Bernadette San Pedro Bayot. Bruno Mars alikulia katika mji wa Waikiki ulio karibu na Honolulu.

Baba yake alikuwa ni wa uzazi wa Puerto Rico na Uyahudi wa Ashkenazi kutoka katika nchi za Ukraine na Hungaria. Mama yake alihamia Hawaii akiwa mtoto akitokea Ufilipino na asili kidogo ya uzao wao ni wa Kihispaniola. Wazazi wake walikuwa wanamuziki. Akiwa na ni miaka miwili baba yake alimpatia la Bruno kutokana na mwanamieleka wakati huo aliyekuwa akiwika Bruno Sammartino.

Mnamo mwaka 2003 Bruno Mars alienda zake Los Angeles  akiwa na dhamira ya kuinua kipaji chake cha muziki. Akiwa hapo alisaini kuwa na Motown Records ambao baadaye alishindwana kasha Mars akasaini mkataba na Atlantic Records mwaka 2009. Mwaka huo huo alikutana na maprodyuza wakali waliofahamika kwa jina la The Smeezingtons ambao walimfanya Bruno Mars aweze kung’ara.

Bruno Mars aliionekana mnamo mwaka 2010 katika “Nothin’ on You” –B.o.B pia track ya Billionaire chini ya Travie McCoy. Hadi sasa Mars ameuza singles zaidi ya milioni 200 na albamu milioni 26 duniani kote hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa best selling artists wa zama zote.

Mnamo mwaka 2011 Mars alionekana katika jarida la TIME kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani. Pia Jarida la Forbes ameonekana katika 100 bora za wasanii kwa miaka tofauti tofauti kuanzia 2013.
,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *