Mfahamu CEO mpya Simba, mrithi wa Senzo Mazingiza na CV yake

September 6, 2020

Mabingwa wa Nchi, Simba SC wameanika CV ya Barbara Gonzalez ambaye walimtangaza kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa klabu.Simba imeanika uwezo wake huo katika kile ambacho anakwenda kukabiliana nacho atakapokuwa ndani ya Simba kama CEO. Miamba hiyo ya soka Tanzania kupitia Bodi yao imeandika kuwa haina shaka hata kidogo hasa kutokana na mapenzi yake katika soka.Sehemu ya maelezo yaliyotolewa na Simba ikimuelezea mwanadada Barbara imesema “Akiwa Mjumbe wa Bodi na Kamati mbalimbali za Simba, aliwezesha majadiliano na FIFA, CAF, Arsenal, Liverpool, Juventus, Porto FC na Everton yote ikiwa na lengo la kutengeneza uhusiano kwaajili ya maendeleo ya vijana na kujenga uwezo katika usimamizi wa kisasa wa mpira wa Miguu. ”Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Simba imeandika kuwa ”Bodi ya Simba inamshukuru Barbara kwa kukubali jukumu hili. Bodi haina shaka kabisa kwamba mapenzi yake ya dhati kwa mpira wa miguu, uelewa wake mkubwa wa masuala muhimu ndani ya Simba, na mahusiano yake mazuri na wadau mbalimbali wa soka nchini yatamsaidia kuisaidia Simba kufikia malengo yake.”Barbara Gonzalez anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa CEO wa Simba SC, Senzo Mbatha Mazingiza aliyetimkia kwa wapinzani wao wa jadi Yanga SC,

Mabingwa wa Nchi, Simba SC wameanika CV ya Barbara Gonzalez ambaye walimtangaza kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa klabu.

Simba imeanika uwezo wake huo katika kile ambacho anakwenda kukabiliana nacho atakapokuwa ndani ya Simba kama CEO. Miamba hiyo ya soka Tanzania kupitia Bodi yao imeandika kuwa haina shaka hata kidogo hasa kutokana na mapenzi yake katika soka.

Sehemu ya maelezo yaliyotolewa na Simba ikimuelezea mwanadada Barbara imesema “Akiwa Mjumbe wa Bodi na Kamati mbalimbali za Simba, aliwezesha majadiliano na FIFA, CAF, Arsenal, Liverpool, Juventus, Porto FC na Everton yote ikiwa na lengo la kutengeneza uhusiano kwaajili ya maendeleo ya vijana na kujenga uwezo katika usimamizi wa kisasa wa mpira wa Miguu. ”

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Simba imeandika kuwa ”Bodi ya Simba inamshukuru Barbara kwa kukubali jukumu hili. Bodi haina shaka kabisa kwamba mapenzi yake ya dhati kwa mpira wa miguu, uelewa wake mkubwa wa masuala muhimu ndani ya Simba, na mahusiano yake mazuri na wadau mbalimbali wa soka nchini yatamsaidia kuisaidia Simba kufikia malengo yake.”

Barbara Gonzalez anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa CEO wa Simba SC, Senzo Mbatha Mazingiza aliyetimkia kwa wapinzani wao wa jadi Yanga SC

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *