Meneja wa Harmonize Afunguka Changamoto za Kazi

September 19, 2020

KATIKA tasnia ya muziki na wanamuziki wakali, huwezi kuacha kumtaja Bosi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide na staa wa muziki Afrika Mashariki, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’. Kuonekana kwa ubora wake, ni kutokana na watu walio nyuma yake wanaomsimamia kama Jembe ni Jembe, Rajab Mchopa na mwanamke ambaye naweza kumuita Malkia wa Nguvu, Beauty Mmari ‘Mjerumani’.Mjerumani amekuwa ni meneja ambaye anasimamia kazi za Harmonize au Harmo kwa kiwango kikubwa na kumfikisha hapo alipo sasa. IJUMAA SHOWBIZ  imefanya mahojiano maalum (exclusive interview) na Mjerumani ambaye amefunguka mengi;KING OF SINGELI 2020!kubwa zaidi ni kuhusiana na kazi za Harmo na jitihada za kumfanya awe mwanamuziki wa kimataifa ‘mtu na nusu’; IJUMAA SHOWBIZ: Hongera kwa kuongeza idadi ya wasanii kwenye Lebo ya Konde Gang Music Worldwide…MJERUMANI:Asante sana.IJUMAA SHOWBIZ: Kama meneja, unalizungumziaje hili la kuongeza idadi ya wasanii? MJERUMANI: Kwetu sisi tumepiga hatua, maana lebo ilianza na msanii mmoja ambaye ni Harmonize, lakini baadaye tukaona hatoshi na ikabidi apate wenzake.Tunamshukuru Mungu, ni vijana wenye vipaji na uelewa mkubwa wa muziki wetu.IJUMAA SHOWBIZ: Mipango iko vipi kuwaendeleza wasanii wapya?MJERUMANI:Mipango ni mingi na kama mnavyoona, ni wasanii wenye vipaji vikubwa, kuna utaratibu tuliyojiwekea katika kutoa kazi zao, nadhani mashabiki zao watazipenda kwa sababu ni kazi kubwa na tukichukua wasanii, ni lazima tuwatengeneze wawe katika ubora tunaoutaka. IJUMAA SHOWBIZ:Utofauti wa Konde Music na lebo nyingine ni upi? MJERUMANI: Muziki wetu si wa ndani tu, ni wa nje ya Afrika kabisa ni muziki wa kimataifa na huwa tuna haki sawa kwa wasanii wote na si Harmonize tu.IJUMAA SHOWBIZ:Harmonize ni mwanamuziki mkubwa, je, unawezaje kumsimamia?MJERUMANI: Nashukuru yeye ana malengo makubwa na ni mwepesi sana kumsimamia kwa sababu anajua ana dira na anataka nini, anajitambua. Tunapeana miongozo na kupitia changamoto kwa pamoja kama meneja na msanii wake na tunaona tunatengeneza muziki wa biashara. IJUMAA SHOWBIZ:Ni vitu gani unaviona kwa msanii wako Harmonize? MJERUMANI: Harmonize anapenda kujifunza na kuwafunza wenziye, pia ni mtu ambaye ukifanya biashara ya muziki, mnabadilishana uzoefu. IJUMAA SHOWBIZ:Wewe kama mwanamke, ni changamoto gani kubwa ambayo umekuwa ukikabiliana nayo katika kumsimamia Harmonize? MJERUMANI: Kwanza jinsia si tatizo, ila ni kujua soko linataka nini. Kama mwanamke na meneja kwa nafasi yangu, nimekuwa nikiweza kukabiliana na mambo mengi yanayomhusu Harmonize na ninaamini tupo vizuri na mambo mengi yanakwenda vizuri, maana tayari yuko katika levo za kimataifa, cha msingi ni kuangalia mipango ikoje na msanii anataka nini, maana biashara ni ngumu na ushindani ni mkubwa.IJUMAA SHOWBIZ: Ishu ya Harmonize kuanguka na kamba pale Uwanja wa Mkapa, unaizungumziaje?MJERUMANI: Kuhusiana na suala la Harmo kuanguka na kamba, ile ni sehemu ya shoo yake, muziki una sanaa ya maonesho ndani yake, ile ni moja ya staili aliyoamua kuingia nayo ili kuwaburudisha mashabiki wake. Nafikiri mashabiki walipata wasiwasi kwa sababu ile hali ya kupanda ngazi hufanywa na watu wenye weledi zaidi. Harmonize ni msanii si mwanajeshi na hana mafunzo ya moja kwa moja kama ninavyosema, huwa ana uthubutu, ila pale hakuanguka na ile kamba inavyoshushwa imebeba mtu na inashuka kwa fosi, ni kawaida.IJUMAA SHOWBIZ: Je, baada ya pale hakuumia? MJERUMANI: Hakuumia na baadaye alikuwa na sherehe ofisini kwake na kesho yake alikwenda kumpokea mchezaji wa timu ya Yanga. IJUMAA SHOWBIZ:Tukirudi kwenye upande wa biashara, Album ya Afro East imeleta mafanikio kiasi gani? MJERUMANI: Kwanza ile album tunamshukuru Mungu, maana tulipitia changamoto la Janga la Corona, imefanya vizuri sokoni na ni moja ya album za wasanii wa Afrika inayofuatiliwa hata ukiangalia kwenye digital platforms (mitandaoni), ni moja ya projekti iliyofanya vizuri sokoni, japo kwa bahati mbaya haikufikia malengo ambayo tulijiwekea na hatukuweza kuwafikishia mashabiki kwa kuipafomu.Imesikilizwa mno na ule ni mtaji tosha, japokuwa tunakuja na kazi nyingine, ambayo itafanya vizuri zaidi.IJUMAA SHOWBIZ:Mapokezi ya ujio wa album nyingine yako vipi, album ya pili itaweza kuipindua Afro East? MJERUMANI: Kila kitu kinafanyika kwa sababu na kuzingatia soko linahitaji nini kwa wakati huo, hatuwezi kusema itaipindua album ya kwanza, maana kila siku Harmonize amekuwa akifanya vitu vya kitofauti, ni mtu wa kujiongeza sana na inayokuja ni kubwa zaidi. IJUMAA SHOWBIZ: Je, mmelenga nini hasa? MJERUMANI: Tumelenga soko la kimataifa zaidi na tuna imani itafanya vizuri ziadi. IJUMAA SHOWBIZ: Kama meneja, malengo yako ni yapi katika kumuendeleza Harmonize mbele zaidi katika miaka mingine ijayo ya muziki wake? MJERUMANI: Natamani Harmonize kama msanii aliyepata fursa ya kufanya muziki na kuwakilisha Afrika, muziki wake ufike mbali zaidi, tunataka awe mtu na nusu na kupitia yeye na wasanii wengine wengi wanaofanya vizuri. IJUMAA SHOWBIZ:Mashabiki wa Harmo watarajie nini makubwa? MJERUMANI: Kama meneja wake, tunaona muziki wake uko mbali kwa sababu amekuwa akitaka kuleta utofauti kwenye industry na tutegemee makubwa maana anajituma sana, anafanya utafiti na kushirikiana na wasanii wenzake vizuri na ana uwezo wa kuvusha malengo ya vijana wa Kitanzania na kuwashika mkono kama tulivyokuwa na wasanii wengine. IJUMAA SHOWBIZ:Kuwasajili wasanii wengine tena kwa spidi, nini malengo? MJERUMANI: Tunatoa fursa ya vijana kupambania ndoto zao, kupitia brandi ya Harmonize ina uthamani wa kuwafikisha wengine mbele, maana tunaangalia ubora wa brandi yake na kuzalisha wengine.IJUMAA SHOWBIZ:Je, kuna uwezekano wa kuongeza wasanii wengine? MJERUMANI: Ndiyo tutegemee Konde Gang itakuwa na wasanii wengine zaidi na hata nje ya Tanzania kama tulivyofanya kwa Skales na inaweza ikawa ni lebo ambayo imesaini msanii kimataifa. IJUMAA SHOWBIZ:Mmeweza kumsaini Skales ambaye ni mwanamuziki mkubwa Nigeria, je, hamkupitia changamoto yoyote? MJERUMANI: Kwanza ifahamike kuwa, Skales na Harmonize ni marafiki wakubwa, wamefanya kolabo kama tatu au nne na Harmonize amekuwa ni shabiki mkubwa wa kazi za Skales. IJUMAA SHOWBIZ: Mtazamo wa Skales kwenye muziki wetu ukoje? MJERUMANI: Skales ni mtu ambaye anapenda sana muziki wa Kitanzania na hata alipokuwa akija, iliturahisishia kutengeneza uhusiano wa kibiashara na ataendelea kutoa projekti nyingi. Kupitia yeye, wasanii wengi watafanya kazi za Nigeria. IJUMAA SHOWBIZ: Je, mipango iko vipi ya Skales na Harmonize kutoa kazi ya pamoja?MJERUMANI:Inategemea na mipango ya lebo na kuangalia soko. IJUMAA SHOWBIZ: Kwa sasa mmepata dili za Harmonize kupiga shoo nje? MJERUMANI: Kwa wenzetu suala la Corona liliwaathiri zaidi na bado hawajawa na utayari wa kupata burudani, bado hatujapata mialiko ya kwenda nje, ila mwakani biashara itarudi.IJUMAA SHOWBIZ:Kama meneja, unalionaje soko la muziki wa Bongo Fleva? MJERUMANI: Soko la Bongo Fleva lipo vizuri Afrika Mashariki, linafanya vizuri na tuna wasanii wakubwa wanaotuwakilisha kama Harmonize na wengine. Soko linakua na limeanza kuwa biashara kubwa, tofauti na nyuma. IJUMAA SHOWBIZ:Je, Studio za Konde Gang zinafanya kazi za wasanii wake tu au hata wa nje ya lebo?MJERUMANI: Kwa sasa tunafanya kazi za Konde Gang na wasanii tofautitofauti, wasanii wetu wako kwenye soko la wasanii wenzao kama marafiki.Waandishi: Happyness Masunga na Khadija Bakari.,

KATIKA tasnia ya muziki na wanamuziki wakali, huwezi kuacha kumtaja Bosi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide na staa wa muziki Afrika Mashariki, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’.

 

Kuonekana kwa ubora wake, ni kutokana na watu walio nyuma yake wanaomsimamia kama Jembe ni Jembe, Rajab Mchopa na mwanamke ambaye naweza kumuita Malkia wa Nguvu, Beauty Mmari ‘Mjerumani’.

Mjerumani amekuwa ni meneja ambaye anasimamia kazi za Harmonize au Harmo kwa kiwango kikubwa na kumfikisha hapo alipo sasa.

 

IJUMAA SHOWBIZ  imefanya mahojiano maalum (exclusive interview) na Mjerumani ambaye amefunguka mengi;

KING OF SINGELI 2020!kubwa zaidi ni kuhusiana na kazi za Harmo na jitihada za kumfanya awe mwanamuziki wa kimataifa ‘mtu na nusu’;

 

IJUMAA SHOWBIZ: Hongera kwa kuongeza idadi ya wasanii kwenye Lebo ya Konde Gang Music Worldwide…

MJERUMANI:Asante sana.

IJUMAA SHOWBIZ: Kama meneja, unalizungumziaje hili la kuongeza idadi ya wasanii?

 

MJERUMANI: Kwetu sisi tumepiga hatua, maana lebo ilianza na msanii mmoja ambaye ni Harmonize, lakini baadaye tukaona hatoshi na ikabidi apate wenzake.Tunamshukuru Mungu, ni vijana wenye vipaji na uelewa mkubwa wa muziki wetu.

IJUMAA SHOWBIZ: Mipango iko vipi kuwaendeleza wasanii wapya?

MJERUMANI:Mipango ni mingi na kama mnavyoona, ni wasanii wenye vipaji vikubwa, kuna utaratibu tuliyojiwekea katika kutoa kazi zao, nadhani mashabiki zao watazipenda kwa sababu ni kazi kubwa na tukichukua wasanii, ni lazima tuwatengeneze wawe katika ubora tunaoutaka.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Utofauti wa Konde Music na lebo nyingine ni upi?

 

MJERUMANI: Muziki wetu si wa ndani tu, ni wa nje ya Afrika kabisa ni muziki wa kimataifa na huwa tuna haki sawa kwa wasanii wote na si Harmonize tu.

IJUMAA SHOWBIZ:Harmonize ni mwanamuziki mkubwa, je, unawezaje kumsimamia?

MJERUMANI: Nashukuru yeye ana malengo makubwa na ni mwepesi sana kumsimamia kwa sababu anajua ana dira na anataka nini, anajitambua. Tunapeana miongozo na kupitia changamoto kwa pamoja kama meneja na msanii wake na tunaona tunatengeneza muziki wa biashara.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Ni vitu gani unaviona kwa msanii wako Harmonize?

 

MJERUMANI: Harmonize anapenda kujifunza na kuwafunza wenziye, pia ni mtu ambaye ukifanya biashara ya muziki, mnabadilishana uzoefu.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Wewe kama mwanamke, ni changamoto gani kubwa ambayo umekuwa ukikabiliana nayo katika kumsimamia Harmonize?

 

MJERUMANI: Kwanza jinsia si tatizo, ila ni kujua soko linataka nini. Kama mwanamke na meneja kwa nafasi yangu, nimekuwa nikiweza kukabiliana na mambo mengi yanayomhusu Harmonize na ninaamini tupo vizuri na mambo mengi yanakwenda vizuri, maana tayari yuko katika levo za kimataifa, cha msingi ni kuangalia mipango ikoje na msanii anataka nini, maana biashara ni ngumu na ushindani ni mkubwa.

IJUMAA SHOWBIZ: Ishu ya Harmonize kuanguka na kamba pale Uwanja wa Mkapa, unaizungumziaje?

MJERUMANI: Kuhusiana na suala la Harmo kuanguka na kamba, ile ni sehemu ya shoo yake, muziki una sanaa ya maonesho ndani yake, ile ni moja ya staili aliyoamua kuingia nayo ili kuwaburudisha mashabiki wake.

 

Nafikiri mashabiki walipata wasiwasi kwa sababu ile hali ya kupanda ngazi hufanywa na watu wenye weledi zaidi. Harmonize ni msanii si mwanajeshi na hana mafunzo ya moja kwa moja kama ninavyosema, huwa ana uthubutu, ila pale hakuanguka na ile kamba inavyoshushwa imebeba mtu na inashuka kwa fosi, ni kawaida.IJUMAA SHOWBIZ: Je, baada ya pale hakuumia?

 

MJERUMANI: Hakuumia na baadaye alikuwa na sherehe ofisini kwake na kesho yake alikwenda kumpokea mchezaji wa timu ya Yanga.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Tukirudi kwenye upande wa biashara, Album ya Afro East imeleta mafanikio kiasi gani?

 

MJERUMANI: Kwanza ile album tunamshukuru Mungu, maana tulipitia changamoto la Janga la Corona, imefanya vizuri sokoni na ni moja ya album za wasanii wa Afrika inayofuatiliwa hata ukiangalia kwenye digital platforms (mitandaoni), ni moja ya projekti iliyofanya vizuri sokoni, japo kwa bahati mbaya haikufikia malengo ambayo tulijiwekea na hatukuweza kuwafikishia mashabiki kwa kuipafomu.Imesikilizwa mno na ule ni mtaji tosha, japokuwa tunakuja na kazi nyingine, ambayo itafanya vizuri zaidi.

IJUMAA SHOWBIZ:Mapokezi ya ujio wa album nyingine yako vipi, album ya pili itaweza kuipindua Afro East?

 

MJERUMANI: Kila kitu kinafanyika kwa sababu na kuzingatia soko linahitaji nini kwa wakati huo, hatuwezi kusema itaipindua album ya kwanza, maana kila siku Harmonize amekuwa akifanya vitu vya kitofauti, ni mtu wa kujiongeza sana na inayokuja ni kubwa zaidi.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Je, mmelenga nini hasa?

 

MJERUMANI: Tumelenga soko la kimataifa zaidi na tuna imani itafanya vizuri ziadi.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Kama meneja, malengo yako ni yapi katika kumuendeleza Harmonize mbele zaidi katika miaka mingine ijayo ya muziki wake?

 

MJERUMANI: Natamani Harmonize kama msanii aliyepata fursa ya kufanya muziki na kuwakilisha Afrika, muziki wake ufike mbali zaidi, tunataka awe mtu na nusu na kupitia yeye na wasanii wengine wengi wanaofanya vizuri.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Mashabiki wa Harmo watarajie nini makubwa?

 

MJERUMANI: Kama meneja wake, tunaona muziki wake uko mbali kwa sababu amekuwa akitaka kuleta utofauti kwenye industry na tutegemee makubwa maana anajituma sana, anafanya utafiti na kushirikiana na wasanii wenzake vizuri na ana uwezo wa kuvusha malengo ya vijana wa Kitanzania na kuwashika mkono kama tulivyokuwa na wasanii wengine.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Kuwasajili wasanii wengine tena kwa spidi, nini malengo?

 

MJERUMANI: Tunatoa fursa ya vijana kupambania ndoto zao, kupitia brandi ya Harmonize ina uthamani wa kuwafikisha wengine mbele, maana tunaangalia ubora wa brandi yake na kuzalisha wengine.IJUMAA SHOWBIZ:Je, kuna uwezekano wa kuongeza wasanii wengine?

 

MJERUMANI: Ndiyo tutegemee Konde Gang itakuwa na wasanii wengine zaidi na hata nje ya Tanzania kama tulivyofanya kwa Skales na inaweza ikawa ni lebo ambayo imesaini msanii kimataifa.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Mmeweza kumsaini Skales ambaye ni mwanamuziki mkubwa Nigeria, je, hamkupitia changamoto yoyote?

 

MJERUMANI: Kwanza ifahamike kuwa, Skales na Harmonize ni marafiki wakubwa, wamefanya kolabo kama tatu au nne na Harmonize amekuwa ni shabiki mkubwa wa kazi za Skales.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Mtazamo wa Skales kwenye muziki wetu ukoje?

 

MJERUMANI: Skales ni mtu ambaye anapenda sana muziki wa Kitanzania na hata alipokuwa akija, iliturahisishia kutengeneza uhusiano wa kibiashara na ataendelea kutoa projekti nyingi. Kupitia yeye, wasanii wengi watafanya kazi za Nigeria.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Je, mipango iko vipi ya Skales na Harmonize kutoa kazi ya pamoja?MJERUMANI:Inategemea na mipango ya lebo na kuangalia soko.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Kwa sasa mmepata dili za Harmonize kupiga shoo nje?

 

MJERUMANI: Kwa wenzetu suala la Corona liliwaathiri zaidi na bado hawajawa na utayari wa kupata burudani, bado hatujapata mialiko ya kwenda nje, ila mwakani biashara itarudi.

IJUMAA SHOWBIZ:Kama meneja, unalionaje soko la muziki wa Bongo Fleva?

 

MJERUMANI: Soko la Bongo Fleva lipo vizuri Afrika Mashariki, linafanya vizuri na tuna wasanii wakubwa wanaotuwakilisha kama Harmonize na wengine. Soko linakua na limeanza kuwa biashara kubwa, tofauti na nyuma.

 

IJUMAA SHOWBIZ:Je, Studio za Konde Gang zinafanya kazi za wasanii wake tu au hata wa nje ya lebo?

MJERUMANI: Kwa sasa tunafanya kazi za Konde Gang na wasanii tofautitofauti, wasanii wetu wako kwenye soko la wasanii wenzao kama marafiki.Waandishi: Happyness Masunga na Khadija Bakari.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *