Membe: Wanaodhani Nitajiondoa Urais Wanaota

September 9, 2020

MGOMBEA urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Bernard Membe, ameweka wazi kuwa hatajiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Membe ameweka wazi msimamo wake huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema kuwa wanaofikiri kuwa atajiondoa katika kinyang’anyiro hicho wanaota ndoto za mchana.“Hatoki mtu hapa! Wale wote wanaodhani kuwa nitajiondoa katika kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, wanaota ndoto za mchana,” ameandika.Aidha  amewataka Watanzania kukaa chonjo na kujiandaa na yatakayojiri kuanzia tarehe 15 Septemba 2020.Ikumbukwe Jumatatu ya wiki hii mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu,  katika ufunguzi wa kampeni kanda ya Unguja, alisema vyama vya upinzani bara vinabidi viuunge mkono mtu anayeweza kuwa mshindani mzuri dhidi ya mgombea wa chama tawala visiwani Zanzibar.,

MGOMBEA urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Bernard Membe, ameweka wazi kuwa hatajiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Membe ameweka wazi msimamo wake huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema kuwa wanaofikiri kuwa atajiondoa katika kinyang’anyiro hicho wanaota ndoto za mchana.

“Hatoki mtu hapa! Wale wote wanaodhani kuwa nitajiondoa katika kinyang’anyiro cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, wanaota ndoto za mchana,” ameandika.

Aidha  amewataka Watanzania kukaa chonjo na kujiandaa na yatakayojiri kuanzia tarehe 15 Septemba 2020.

Ikumbukwe Jumatatu ya wiki hii mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu,  katika ufunguzi wa kampeni kanda ya Unguja, alisema vyama vya upinzani bara vinabidi viuunge mkono mtu anayeweza kuwa mshindani mzuri dhidi ya mgombea wa chama tawala visiwani Zanzibar.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *