Membe awashiwa moto na Mariam Ditopile kwa kwenda kucheki afya nje ya nchi, on September 16, 2020 at 6:00 am

September 16, 2020

 Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Mariam Ditopile amemvaa mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Benard Membe kuwa iwapo atashinda urais atautumia kusafiri nje ya nchi kwa maslahi yake binafsi kwa kigezo cha kutibiwa.” Nimemsikia akisema alienda Dubai kwa ajili ya kuchekiwa afya yake, hii inashangaza Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana kwenye sekta ya Afya, tuna Vituo vya Afya kila mahali, Hospitali za Wilaya za kutosha, Hospitali kubwa kila kanda zenye vifaa vya kisasa leo mtu anaenda kucheki afya nje ya nchi na hajawa Rais akipewa nchi si ndo atahamia kabisa?Rais Magufuli amejitahidi kusitisha safari za nje zisizo na ulazima, yeye mwenye hajawahi kwenda kuchekiwa afya nje ya nchi achilia mbali kutibiwa, Membe yeye kwenda kupima homa tu anaenda Dubai, hii imewaonesha watanzania kuwa yeye ni kiongozi wa aina gani na hakika watamkataa kwa kishindo Oktoba 28,” Amesema Mariam Ditopile.,

 

Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Mariam Ditopile amemvaa mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Benard Membe kuwa iwapo atashinda urais atautumia kusafiri nje ya nchi kwa maslahi yake binafsi kwa kigezo cha kutibiwa.

” Nimemsikia akisema alienda Dubai kwa ajili ya kuchekiwa afya yake, hii inashangaza Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana kwenye sekta ya Afya, tuna Vituo vya Afya kila mahali, Hospitali za Wilaya za kutosha, Hospitali kubwa kila kanda zenye vifaa vya kisasa leo mtu anaenda kucheki afya nje ya nchi na hajawa Rais akipewa nchi si ndo atahamia kabisa?

Rais Magufuli amejitahidi kusitisha safari za nje zisizo na ulazima, yeye mwenye hajawahi kwenda kuchekiwa afya nje ya nchi achilia mbali kutibiwa, Membe yeye kwenda kupima homa tu anaenda Dubai, hii imewaonesha watanzania kuwa yeye ni kiongozi wa aina gani na hakika watamkataa kwa kishindo Oktoba 28,” Amesema Mariam Ditopile.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *