Membe atoa msimamo wake ugombea urais,Hata mninyonge, wabunge 32 siwataji

October 19, 2020

Mimi bado ni mgombea urais halali wa chama cha ACT-Wazalendo na nitakipeleka chama changu kwenye Uchaguzi Mkuu October 28”, alisema Membe kwa kujiamini na kuongeza kuwa ACT-Wazalendo ni chama chetu, ni chama kizuri kabisa na kinasera nzuri”.

Aidha, Membe amejitapa kwa kusema kwamba “Mazingira ya wapinzani kuiondoa CCM madarakani yameiva. Nilikuwa tayari kuiondoa serikali hii madarakani wakati nikiwa Chama cha Mapinduzi wanabahati yao walinifukuza”

“Mimi nilikuwa CCM nikatataka kukabiliana na rais aliyepo madarakani peke yangu kumuondoa, lakini washukuru walinifukuza, tulijianda na wana CCM wenzangu, achilia mbali tulikuwa watu 6 tuliokuwa tayari kuiondoa serikali madarakani, mimi nilikuwa na wabunge 78, kwa bahati mbaya 46 wamefyekwa lakini wako CCM, 32 wamebaki hata mkininyonga siwezi kuwataja kwa sababu watatumbuliwa tu”, amesimulia Membe.

Aidha Membe ameongeza kuwa, “Kuungana kwa vyama vya upinzani ni lazima chama tawala kipasuke ili kundi la pili lije upande wa pili ili kusaidia chama tawala kuangushwa CCM mwisho wake umefika na tunawaondoa madarakani Oktoba 28”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *