Mdahalo kati ya Trump na Biden wafutwa

October 11, 2020

Mdahalo kati ya Biden na Trump uliokuwa umepangwa kufanyika 15 Oktoba umefutwa.

Tume ya Mdahalo wa wagombea Urais nchini Marekani imetangaza kufuta mdahalo wa pili kati ya Donald Trump na Joe Biden uliopaswa kufanyika tarehe 15 mwezi Oktoba, ikiwa imebaki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu Novemba 3.

Mabadiliko haya yamekuja baada ya Donald Trump kutangaza kukutwa na maambukizi ya corona siku chache zilizopita.

Tume hiyo hapo awali ikuwa imependekeza mdahalo ufanyike kwa njia ya hadhara ambapo Biden na Trump wangekaa mbali mbali kwa ajili ya usalama na wanachi wangepata fursa ya kuuliza maswali moja kwa moja kwa wagombea

Trump alikataa mdahalo huo na kusema kuwa hauleti maana.

Hata hivyo, Wamarekani kwa sasa wanasubiri kwa hamu mdahalo wa tatu na wa mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Nashville, Tennessee, tarehe 22 Oktoba.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *