Mchungahela ahaidi kuboresha elimu kwa kutoa komputa bure mashuleni, on September 7, 2020 at 8:00 am

September 7, 2020

    Na Hamisi Nasri,Masasi     MGOMBEA ubunge Jimbo la Lulindi,Chama cha Mapinduzi, (CCM) Issa Mchungahela ameahidi akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atatoa kompyuta mpakato(Laptop)bule katika shule zote za sekondari na msingi ili wanafunzi waweze kusoma kwa njia ya teknolojia na mawasiliano (TEHAMA)     Aliyasema hayo jana wilayani Masasi alipokuwa akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo katika uzinduzi wa kampeni zake, uzinduzi huo ambao ulifanyika katika kata ya Mnavila, kijiji cha Mnavila wilayani hapa.    Mchungahela alisema iwapo akichaguliwa kuwa mbunge kipaumbele cha kwanza ambacho ataanzanacho ni kugawa kompyuta mpakato katika shule zote za msingi na sekondari ili wanafunzi wanaosoma katika shule zilizopo kwenye jimbo hilo waweze kusoma kwa kutumia vifaa hivyo.     Alisema baada ya kugawa kompyuta hizo pia atalazimika kuleta walimu wakutosha wenye uweledi wa kutumia compyuta kwa ajili ya kufundisha wanafunzi kwenye shule hizo ili kila mwanafunzi anapomaliza elimu aweze kutumia kompyuta kwa ufanisi mkubwa.  “Mkinichagua kuwa mbunge wa jimbo hili nitahakikisha katika kila shule ya sekondari kunakuwa na kompyuta ili wanafunzi wetu hawa waweze kusoma kwa njia ya kompyuta na kama hakutakuwa na walimu hata mimi mwenyewe nitaingia farasani kufundisha,”alisema Mchungahela    Mchunga alisema jambo lingine ambalo atalifanya ni kuboressha hali ya miundombinu ya barabara ambazo kwa sasa baadhi ya barabara zipo katika hali ya mbaya     Alisema kipaumbele kingine cha kutekeleza ni kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja, huduma ya maji ambapo baadhi ya vijiji havina kabisa huduma ya maji hivyo akichaguliwa atahakikisha huduma hiyo inapatikana kwa haraka.   Alisema katika jimbo la Lulindi kuna miradi mingi ya maji ambayo ililetwa lakini changushangaza miradi hiyo ilishindwa kutekelezwa kutokana na usimamizi mbovu hivyo akiwa mbunge miradi hiyo yote ataifufua na kutoa maji kwa wananchi.   Mchungahela alisema katika jimbo la Lulindi kuna jumla ya kata 18 hivyo kila kata lazima kuwe na huduma zote za msingi ambazo zinakosekana ili ndani ya miaka mitano atakayokuwa amekuwa mbunge awe amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo.   Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara,Yusuf Mnanalia alisema katika jimbo la Lulindi serikali imetumia zaidi ya 6.1 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi shule, maji,vituo vya afya na Zahanati.  Alisema hivyo wanawataka wananchi wa jimbo hilo kutofanya makosa ifikapo oktoba 28 kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kura hiyo kumchagua raisi Dk. John Magufuli na mbunge ambaye ni Mchungahela ili kwa pamoja waweze kuleta maendeleo kwa jimbo la Lilindi.,

   

Na Hamisi Nasri,Masasi  

   MGOMBEA ubunge Jimbo la Lulindi,Chama cha Mapinduzi, (CCM) Issa Mchungahela ameahidi akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atatoa kompyuta mpakato(Laptop)bule katika shule zote za sekondari na msingi ili wanafunzi waweze kusoma kwa njia ya teknolojia na mawasiliano (TEHAMA) 

    Aliyasema hayo jana wilayani Masasi alipokuwa akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo katika uzinduzi wa kampeni zake, uzinduzi huo ambao ulifanyika katika kata ya Mnavila, kijiji cha Mnavila wilayani hapa.

    Mchungahela alisema iwapo akichaguliwa kuwa mbunge kipaumbele cha kwanza ambacho ataanzanacho ni kugawa kompyuta mpakato katika shule zote za msingi na sekondari ili wanafunzi wanaosoma katika shule zilizopo kwenye jimbo hilo waweze kusoma kwa kutumia vifaa hivyo.

     Alisema baada ya kugawa kompyuta hizo pia atalazimika kuleta walimu wakutosha wenye uweledi wa kutumia compyuta kwa ajili ya kufundisha wanafunzi kwenye shule hizo ili kila mwanafunzi anapomaliza elimu aweze kutumia kompyuta kwa ufanisi mkubwa.

  “Mkinichagua kuwa mbunge wa jimbo hili nitahakikisha katika kila shule ya sekondari kunakuwa na kompyuta ili wanafunzi wetu hawa waweze kusoma kwa njia ya kompyuta na kama hakutakuwa na walimu hata mimi mwenyewe nitaingia farasani kufundisha,”alisema Mchungahela 

   Mchunga alisema jambo lingine ambalo atalifanya ni kuboressha hali ya miundombinu ya barabara ambazo kwa sasa baadhi ya barabara zipo katika hali ya mbaya 

    Alisema kipaumbele kingine cha kutekeleza ni kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja, huduma ya maji ambapo baadhi ya vijiji havina kabisa huduma ya maji hivyo akichaguliwa atahakikisha huduma hiyo inapatikana kwa haraka.

   Alisema katika jimbo la Lulindi kuna miradi mingi ya maji ambayo ililetwa lakini changushangaza miradi hiyo ilishindwa kutekelezwa kutokana na usimamizi mbovu hivyo akiwa mbunge miradi hiyo yote ataifufua na kutoa maji kwa wananchi.

   Mchungahela alisema katika jimbo la Lulindi kuna jumla ya kata 18 hivyo kila kata lazima kuwe na huduma zote za msingi ambazo zinakosekana ili ndani ya miaka mitano atakayokuwa amekuwa mbunge awe amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo.

   Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara,Yusuf Mnanalia alisema katika jimbo la Lulindi serikali imetumia zaidi ya 6.1 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi shule, maji,vituo vya afya na Zahanati.

  Alisema hivyo wanawataka wananchi wa jimbo hilo kutofanya makosa ifikapo oktoba 28 kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kura hiyo kumchagua raisi Dk. John Magufuli na mbunge ambaye ni Mchungahela ili kwa pamoja waweze kuleta maendeleo kwa jimbo la Lilindi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *