Mchazaji Marcus Rashford Apewa TUZO na Malkia wa Uingereza

October 12, 2020

 

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Marcus Rashford,22, amepewa tuzo ya MBE na Malkia wa Uingereza kwa juhudi zake katika kusaidia kutatua tatizo la umaskini wa chakula kwa watoto wenye mahitaji ya chakula nchini humo wakati huu wa janga la COVID-19.

Tuzo ya MBE Maana yake ni ‘Member of the Order of the British Empire’ ni tuzo ya kiwango cha tatu cha juu katika tuzo hizo kutoka kwa British Empire. Ya kwanza ni CBE ‘Commander of the Order of the British Empire’ na ya pili ni OBE ‘Officer of the Order of the British Empire’.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *