Mbwana Samatta Afunguka Kuhusu Astona Villa – Siwezi Kumlaumu mtu (+Video)

October 5, 2020

 

Mshambuliaji wa klabu ya Fenerbahce Mbwana Samatta amesema kamwe hawezi kumlaumu mtu yoyote kwa kile kilichotokea akiwa Aston Villa.

Samatta ameyasema hayo wakati akijibu swali la Wandishi wa Habari, kwa kushindwa kutimiza matarajio ya Aston Villa hasa kwenye upande wa kufunga magoli baada ya kujiunga nayo akitokea Genk, pengine sababu ilikuwa ni nini ama Kocha wake mpya kumpatia majukumu mengine ndani ya uwanja.

”Siwezi kumlaumu mtu yoyote kuhusu kile kilichotokea Aston Villa, kwangu mimi ni uzoefu mzuri kuwanao kabla ya kujiunga na klabu bora kama Fenerbahce, nalichukulia ‘positive’ na nafikiri Mungu alijua nilitakiwa kupitia Aston Villa kabla ya kujiunga na Fenerbahce”- Samatta

Akijibu swali aliloulizwa kuwa baada ya kuwepo kwa taarifa zinazo mhusu, kukawa na tetesi Dar Es Salaam kwamba anapendelea kusalia England je sababu gani zilimpelekea kuichagua Fenerbahce ? Samatta amesema ”Kama nilivyosema kwenye swali la kwanza, Fenerbahce ni klabu kubwa duniani, na unapopata fursa ya kuja kwenye timu kama Fenerbahce ni vigumu kukata. Hivyo hiyo ilikuwa fursa iliyokuja kwangu na nimekuwa mwenye furaha kuungana nao, kwasababu nafahamu ni klabu nzuri yenye mashabiki waajabu.”

”Nimeanza mpira kama watoto wengine, nimecheza kuanzia mtaani, nikapata nafasi klabu ya chini na kupata nafasi ya kuichezea moja ya klabu kubwa Tanzania Simba kisha nikaelekea TP Mazembe ya Congo kabla ya kwenda Ubelgiji. Ndiyo ninakipaji ila naamini Mungu amenichagua.”- Samatta ameyasema hayo alipoulizwa namna alivyoanza mchezo wa soka.

View this post on Instagram

#FumoUpdates SAMATTA AKIFUNGUKA KUHUSU ASTON VILLA – SIMLAUMU MTU YOYOTE (3) . Mshambuliaji wa klabu ya Fenerbahce Mbwana Samatta amesema kamwe hawezi kumlaumu mtu yoyote kwa kile kilichotokea akiwa Aston Villa. Samatta ameyasema hayo wakati akijibu swali la Wandishi wa Habari, kwa kushindwa kutimiza matarajio ya Aston Villa hasa kwenye upande wa kufunga magoli baada ya kujiunga nayo akitokea Genk, pengine sababu ilikuwa ni nini ama Kocha wake mpya kumpatia majukumu mengine ndani ya uwanja. ”Siwezi kumlaumu mtu yoyote kuhusu kile kilichotokea Aston Villa, kwangu mimi ni uzoefu mzuri kuwanao kabla ya kujiunga na klabu bora kama Fenerbahce, nalichukulia ‘positive’ na nafikiri Mungu alijua nilitakiwa kupitia Aston Villa kabla ya kujiunga na Fenerbahce”- Samatta Akijibu swali aliloulizwa kuwa baada ya kuwepo kwa taarifa zinazo mhusu, kukawa na tetesi Dar Es Salaam kwamba anapendelea kusalia England je sababu gani zilimpelekea kuichagua Fenerbahce ? Samatta amesema ”Kama nilivyosema kwenye swali la kwanza, Fenerbahce ni klabu kubwa duniani, na unapopata fursa ya kuja kwenye timu kama Fenerbahce ni vigumu kukata. Hivyo hiyo ilikuwa fursa iliyokuja kwangu na nimekuwa mwenye furaha kuungana nao, kwasababu nafahamu ni klabu nzuri yenye mashabiki waajabu.” ”Nimeanza mpira kama watoto wengine, nimecheza kuanzia mtaani, nikapata nafasi klabu ya chini na kupata nafasi ya kuichezea moja ya klabu kubwa Tanzania Simba kisha nikaelekea TP Mazembe ya Congo kabla ya kwenda Ubelgiji. Ndiyo ninakipaji ila naamini Mungu amenichagua.”- Samatta ameyasema hayo alipoulizwa namna alivyoanza mchezo wa soka.

A post shared by Hamza Fumo (@fumo255) on Oct 4, 2020 at 8:36am PDT

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *