Mbozi waanzisha mfumo mpya kutatua vifo vya mama na mtoto, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on August 30, 2020 at 1:00 pm

August 30, 2020

Na, Baraka Messa, Mbozi.ILI kukabiliana na Vifo vya akina mama , watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano Halmashuri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe imeanzisha mfumo mahususi wa kushirikisha viongozi wa Vijiji, Kata, Madiwani ,Viongozi wa Mitaa na wananchi namna ya kushiriki na kuzingatia elimu ya afya baada ya mama kubainika kuwa na ujauzito.Akiongea na mwandishi wa Muungwana Mratibu wa huduma za afya uzazi na mtoto Wilaya ya Mbozi Alexia Nonjela alisema kutokana na changamoto ya vifo vya watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara na vyombo vya habari pamoja na idara ya afya wameanzisha Mfumo uitwao UTURO Modal wakilenga kukomesha kabisa vifo hivyo.Alisema UTURO Modal ni mfumo walio uchukua katika Halmashauri ya Wilaya Mbalali Mkoani Mbeya ambapo kwa kiasi kikubwa Halmashauri hiyo walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kushirikisha jamii katika kuhakikisha wajawazito wote chini ya miezi mitatu kuanza kuhudhuria Kliniki na kukomesha kabisa vifo vya mama na mtoto.Nnonjela alisema mkakati huo unashirikisha viongozi wa mitaa , vijiji , Madiwani na wananchi ambapo kwa pamoja wanachagua wanawake watatu maarufu kama (Makomando) wanaojua kusoma na kuandika wenye sifa za kujitolea , kuwa na siri,  upendo na waaminifu ambao hutoa elimu na taarifa zote za akina mama wanaopata ujauzito ikiwa ni kuhakikisha wanahudhuria Kliniki baada ya miezi mitatu ya mwanzo. Alisema kitendo cha viongozi hao wanaochaguliwa na wananchi wamaeneo husika kimeonyesha matokeo chanya kwa kiasi kikubwa ndani ya muda mfupi walioanza kwa kuwa wamewasaidia kuhamasisha wajawazito wengi kuhudhuria Kliniki mapema na kupunguza vifo vya mama na mtoto ambvyo vilikuwa vinasbabishwa na kuchelewa kuanza kuhudhuria Kliniki.‘’Tulizindua huu mkakati mwezi  Februari mwaka huu 2020, ndani ya muda mfupi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo kablaya kuanza UTURO modal vifo vya akina mama kuanzia januari mwaka huu mpaka kufika machi tulikuwa na akina mama waliofariki kutokana na matatizo ya uzazi na siku 42 kabla ya kujifungua walikuwa watano,Lakini robo ya april mpaka juni akina mama waliofariki walikuwa wawili hivyo jumla kufikia saba katika robo mbili, wakati huo huo walio kuja kliniki chini ya wiki 12 januari mpaka machi ilikuwa asilimia 38, lakini april mpaka juni iliongezeka nakufikia asilimia 45.5’ alisema Nnonjela.Aliongeza kuwa waliojifungulia kituoni kabla ya kuanza Uturo januari mpaka machi ilikuwa asilimia 78 lakini baada ya kuanza uturo waliojifungulia kituoni idadi imeongezeka na kufikia asilimia 82.5.Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Adalberth Haule alisema Mfumo wa UTURO kutokana na matokeo mazuri ambayo yalipatikana Mbalali Mkoani Mbeya kwa kukomesha kabisa vifo vya akina mama na mtoto ndani ya miaka 22, Wizara ya Afya tayari upo mbioni kurasimishwa nchi nzima ili kutatua kabisa vifo vya akina mama na mtoto.Alisema Mbozi wakishirikiana na ofisi ya Mkurugenzi ,Mkuu pamoja na ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya wameamua kutekeleza kwa vyanzo vya mapato ya ndani kwa ajili ya kuokoa hivyo vifo vya mama na mtoto.“UTURO imeanza kuleta matokeo chanya kwani mwaka jana 2019 pekee watoto wachanga walifariki 217, akina mama 15 walifariki , lakini mpaka sasa mabadiliko tunayaona kuna mabadiliko makubwa ukilinganisha na mwaka jana kwa hizi robo mbili tulizofanya kazi” alisema Muuguzi Haule.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi Hanji Godiogodi alisema mfumo huo utatatua kwa kiasi kibwa cha vifo vya mama na mtoto ambavyo kwa kiasi kikubwa vilikuwa vinatokea Mbozi hasa sehemu za vijijini.Alisema mfumo huo pia umekuwa ukiathiriwa na baadhi ya wanasiasa kuingiza Siasa katika jambo hilo muhimu na kupelekea baadhiya wananchi kuanza kuwakata waliochaguliwa kusimamia kutoa elimu na kuwafuatilia akina mama wote wanaopata ujauzito katika maeneo yao husika.,

Na, Baraka Messa, Mbozi.

ILI kukabiliana na Vifo vya akina mama , watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano Halmashuri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe imeanzisha mfumo mahususi wa kushirikisha viongozi wa Vijiji, Kata, Madiwani ,Viongozi wa Mitaa na wananchi namna ya kushiriki na kuzingatia elimu ya afya baada ya mama kubainika kuwa na ujauzito.

Akiongea na mwandishi wa Muungwana Mratibu wa huduma za afya uzazi na mtoto Wilaya ya Mbozi Alexia Nonjela alisema kutokana na changamoto ya vifo vya watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara na vyombo vya habari pamoja na idara ya afya wameanzisha Mfumo uitwao UTURO Modal wakilenga kukomesha kabisa vifo hivyo.

Alisema UTURO Modal ni mfumo walio uchukua katika Halmashauri ya Wilaya Mbalali Mkoani Mbeya ambapo kwa kiasi kikubwa Halmashauri hiyo walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kushirikisha jamii katika kuhakikisha wajawazito wote chini ya miezi mitatu kuanza kuhudhuria Kliniki na kukomesha kabisa vifo vya mama na mtoto.

Nnonjela alisema mkakati huo unashirikisha viongozi wa mitaa , vijiji , Madiwani na wananchi ambapo kwa pamoja wanachagua wanawake watatu maarufu kama (Makomando) wanaojua kusoma na kuandika wenye sifa za kujitolea , kuwa na siri,  upendo na waaminifu ambao hutoa elimu na taarifa zote za akina mama wanaopata ujauzito ikiwa ni kuhakikisha wanahudhuria Kliniki baada ya miezi mitatu ya mwanzo.

 Alisema kitendo cha viongozi hao wanaochaguliwa na wananchi wamaeneo husika kimeonyesha matokeo chanya kwa kiasi kikubwa ndani ya muda mfupi walioanza kwa kuwa wamewasaidia kuhamasisha wajawazito wengi kuhudhuria Kliniki mapema na kupunguza vifo vya mama na mtoto ambvyo vilikuwa vinasbabishwa na kuchelewa kuanza kuhudhuria Kliniki.

‘’Tulizindua huu mkakati mwezi  Februari mwaka huu 2020, ndani ya muda mfupi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo kablaya kuanza UTURO modal vifo vya akina mama kuanzia januari mwaka huu mpaka kufika machi tulikuwa na akina mama waliofariki kutokana na matatizo ya uzazi na siku 42 kabla ya kujifungua walikuwa watano,

Lakini robo ya april mpaka juni akina mama waliofariki walikuwa wawili hivyo jumla kufikia saba katika robo mbili, wakati huo huo walio kuja kliniki chini ya wiki 12 januari mpaka machi ilikuwa asilimia 38, lakini april mpaka juni iliongezeka nakufikia asilimia 45.5’ alisema Nnonjela.

Aliongeza kuwa waliojifungulia kituoni kabla ya kuanza Uturo januari mpaka machi ilikuwa asilimia 78 lakini baada ya kuanza uturo waliojifungulia kituoni idadi imeongezeka na kufikia asilimia 82.5.

Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Adalberth Haule alisema Mfumo wa UTURO kutokana na matokeo mazuri ambayo yalipatikana Mbalali Mkoani Mbeya kwa kukomesha kabisa vifo vya akina mama na mtoto ndani ya miaka 22, Wizara ya Afya tayari upo mbioni kurasimishwa nchi nzima ili kutatua kabisa vifo vya akina mama na mtoto.

Alisema Mbozi wakishirikiana na ofisi ya Mkurugenzi ,Mkuu pamoja na ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya wameamua kutekeleza kwa vyanzo vya mapato ya ndani kwa ajili ya kuokoa hivyo vifo vya mama na mtoto.

“UTURO imeanza kuleta matokeo chanya kwani mwaka jana 2019 pekee watoto wachanga walifariki 217, akina mama 15 walifariki , lakini mpaka sasa mabadiliko tunayaona kuna mabadiliko makubwa ukilinganisha na mwaka jana kwa hizi robo mbili tulizofanya kazi” alisema Muuguzi Haule.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi Hanji Godiogodi alisema mfumo huo utatatua kwa kiasi kibwa cha vifo vya mama na mtoto ambavyo kwa kiasi kikubwa vilikuwa vinatokea Mbozi hasa sehemu za vijijini.

Alisema mfumo huo pia umekuwa ukiathiriwa na baadhi ya wanasiasa kuingiza Siasa katika jambo hilo muhimu na kupelekea baadhiya wananchi kuanza kuwakata waliochaguliwa kusimamia kutoa elimu na kuwafuatilia akina mama wote wanaopata ujauzito katika maeneo yao husika.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *