Mbosso Alamba Dili Nono

September 17, 2020

MWANAMUZIKI maarufu wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi (WCB), Mbwana Yusuph Kilungi maarufu kwa jina la Mbosso, ametangazwa kuwa Balozi wa Kampuni ya Tanga Fresh inayojihusisha na utengenezaji wa maziwa, kwa mkataba wa mwaka mmoja.Akizungumza na vyombo vya habari leo Alhamisi, Septemba 17, 2020, jijini Dar es Salaam, wakati wa utambulisho huo, Ofisa Masoko wa Tanga Fresh, Ally Sechonge, amesema umefika wakati sasa vijana watambue umuhimu wa kunywa maziwa kwa afya yao.“Leo ni siku  muhimu kwa kampuni yetu, tuna furaha kumtambulisha kwenu Mbosso kuwa Balozi wa Tanga Fresh, tunamkaribisha sana katika familia yetu na tunaamini ataipeperusha vyema bendera ya Tanga Fresh,” amesema.Ameongeza kwamba kutokana na utafiti walioufanya, wamebaini moja ya visababishi ambavyo vinaifanya jamii kutokunywa maziwa ya kutosha, ambayo ni watuwengi hawana utamaduni wa kunywa maziwa.“Tumeshindwa kutengenezwa na wazazi wetu, tunataka kutengeneza utamaduni huo kwa vizazi vinavyokuja. Faida za kunywa maziwa watu wazima wanaweza wakashindwa kuziona, hivyo tunataka kuwabadilisha vijana wawe wanakunywa vitu vyenye faida katika miili yao, waache kunywa vinywaji vyenye kabohaidreti pekee,” alisisitiza.Aidha, ameongeza kuwa vijana watakapokuwa wanakunywa maziwa kwa kuwa bado wanaendelea kukua, faida na matokeo katika miili na ngozi zao watayaona“Licha ya kunywa vinywaji vingine vyenye sukari, bado wanahitaji kunywa maziwa kwa kuwa wanajenga miili yao, katika hili tunataka kupelekea ujumbe kwa vijana,” aliendelea kufafanua.Amesema kampuni yake wameamua kumpa ubalozi Mbosso kwa kuwa anaweza kufikisha ujumbe kwa vijana, pia ni mzazi mchanga.“Tunataka kuongea na vijana wanywe maziwa lakini tunataka kuanza kuwafundisha watoto kunywa maziwa tumemchukua kwa kuwa tunataka kuongea na wazazi ambao wanataka kujenga familia sasa, pia tumegundua atakuwa balozi mzuri kwetu,” aliongeza.Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Fresh, Innocent Mushi, amesema kampuni hiyo imeboresha bidhaa zake kwa sasa na kuongeza kwamba,  “Tanga Fresh itaendelea kuboresha bidhaa zake na huduma zake katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kuhakikisha tunaendelea kubakia kuwa chaguo namba moja la watumiaji wa bidhaa za maziwa Tanzania.” ,

MWANAMUZIKI maarufu wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi (WCB), Mbwana Yusuph Kilungi maarufu kwa jina la Mbosso, ametangazwa kuwa Balozi wa Kampuni ya Tanga Fresh inayojihusisha na utengenezaji wa maziwa, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Alhamisi, Septemba 17, 2020, jijini Dar es Salaam, wakati wa utambulisho huo, Ofisa Masoko wa Tanga Fresh, Ally Sechonge, amesema umefika wakati sasa vijana watambue umuhimu wa kunywa maziwa kwa afya yao.

“Leo ni siku  muhimu kwa kampuni yetu, tuna furaha kumtambulisha kwenu Mbosso kuwa Balozi wa Tanga Fresh, tunamkaribisha sana katika familia yetu na tunaamini ataipeperusha vyema bendera ya Tanga Fresh,” amesema.

Ameongeza kwamba kutokana na utafiti walioufanya, wamebaini moja ya visababishi ambavyo vinaifanya jamii kutokunywa maziwa ya kutosha, ambayo ni watuwengi hawana utamaduni wa kunywa maziwa.

“Tumeshindwa kutengenezwa na wazazi wetu, tunataka kutengeneza utamaduni huo kwa vizazi vinavyokuja. Faida za kunywa maziwa watu wazima wanaweza wakashindwa kuziona, hivyo tunataka kuwabadilisha vijana wawe wanakunywa vitu vyenye faida katika miili yao, waache kunywa vinywaji vyenye kabohaidreti pekee,” alisisitiza.

Aidha, ameongeza kuwa vijana watakapokuwa wanakunywa maziwa kwa kuwa bado wanaendelea kukua, faida na matokeo katika miili na ngozi zao watayaona

“Licha ya kunywa vinywaji vingine vyenye sukari, bado wanahitaji kunywa maziwa kwa kuwa wanajenga miili yao, katika hili tunataka kupelekea ujumbe kwa vijana,” aliendelea kufafanua.

Amesema kampuni yake wameamua kumpa ubalozi Mbosso kwa kuwa anaweza kufikisha ujumbe kwa vijana, pia ni mzazi mchanga.

“Tunataka kuongea na vijana wanywe maziwa lakini tunataka kuanza kuwafundisha watoto kunywa maziwa tumemchukua kwa kuwa tunataka kuongea na wazazi ambao wanataka kujenga familia sasa, pia tumegundua atakuwa balozi mzuri kwetu,” aliongeza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Fresh, Innocent Mushi, amesema kampuni hiyo imeboresha bidhaa zake kwa sasa na kuongeza kwamba,  “Tanga Fresh itaendelea kuboresha bidhaa zake na huduma zake katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kuhakikisha tunaendelea kubakia kuwa chaguo namba moja la watumiaji wa bidhaa za maziwa Tanzania.” 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *