Mboso alamba ubalozi wa kampuni ya Tanga Fresh, on September 17, 2020 at 1:00 pm

September 17, 2020

 Mwanamuziki kutoka lebo ya Wasafi (WCB) Mbwana Yusuph Kilungi maarufu Mbosso_ ameteuliwa kuwa balozi wa kampuni ya Tanga Fresh kwa kipindi cha mwaka mmoja.Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa utambulisho huo, Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Ally Sechonge amesema umefika wakati sasa vijana watambue umuhimu wa kunywa maziwa kwa afya yao.“Leo ni siku ya muhimu kwa kampuni yetu, tunafurahia kumtambulisha kwenu Mbosso kuwa balozi wa Tanga Fresh. Ni matumaini yetu ataipeperusha vyema bendera ya Tanga Fresh na tunamkaribisha sana katika familia yetu.” Amesema Sechonge.Amesema kulingana na utafiti ambao Tanga Fresh wamefanya moja ya visababishi ambavyo vinaifanya jamii kutokunywa maziwa ya kutosha, wengi hawana utamaduni wa kunywa maziwa.“Tumeshindwa kutengenezwa na wazazi wetu, tunataka kutengeneza utamaduni huo kwa vizazi vinavyokuja. Zile faida za maziwa watu wazima wanaweza wakashindwa kuziona kwa hiyo tunataka kuwabadilisha vijana wawe wanakunywa vitu vyenye faida katika miili yao, waache kunywa vinywaji vyenye kabohaidreti pekee.”Amesema vijana watakapokuwa wanakunywa maziwa kwa kuwa bado wanaendelea kukua faida na matokeo katika miili na ngozi zao watayaona.“Licha ya kunywa vinywaji vingine vyenye sukari, bado wanahitaji kunywa maziwa kwa kuwa wanajenga miili yao tunataka kupelekea ujumbe kwa vijana.”Sechonge amesema wameamua kumpa ubalozi Mbosso kwa kuwa anaweza kufikisha ujumbe kwa vijana pia ni mzazi mchanga.“Tunataka kuongea na vijana wanywe maziwa lakini tunataka kuanza kuwafundisha watoto kunywa maziwa tumemchukua kwa kuwa tunataka kuongea na wazazi ambao wanataka kujenga familia sasa, pia tumegundua atakuwa balozi mzuri kwetu.”Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Fresh, Innocent Mushi amesema kampuni hiyo imeboresha bidhaa zake kwa sasa.“Tanga Fresh itaendelea kuboresha bidhaa zake na huduma zake katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kuhakikisha tunaendelea kubakia kuwa chaguo namba moja la watumiaji wa bidhaa za maziwa Tanzania.” Amesema Mushi.,

 

Mwanamuziki kutoka lebo ya Wasafi (WCB) Mbwana Yusuph Kilungi maarufu Mbosso_ ameteuliwa kuwa balozi wa kampuni ya Tanga Fresh kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa utambulisho huo, Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Ally Sechonge amesema umefika wakati sasa vijana watambue umuhimu wa kunywa maziwa kwa afya yao.
“Leo ni siku ya muhimu kwa kampuni yetu, tunafurahia kumtambulisha kwenu Mbosso kuwa balozi wa Tanga Fresh. Ni matumaini yetu ataipeperusha vyema bendera ya Tanga Fresh na tunamkaribisha sana katika familia yetu.” Amesema Sechonge.
Amesema kulingana na utafiti ambao Tanga Fresh wamefanya moja ya visababishi ambavyo vinaifanya jamii kutokunywa maziwa ya kutosha, wengi hawana utamaduni wa kunywa maziwa.
“Tumeshindwa kutengenezwa na wazazi wetu, tunataka kutengeneza utamaduni huo kwa vizazi vinavyokuja. Zile faida za maziwa watu wazima wanaweza wakashindwa kuziona kwa hiyo tunataka kuwabadilisha vijana wawe wanakunywa vitu vyenye faida katika miili yao, waache kunywa vinywaji vyenye kabohaidreti pekee.”
Amesema vijana watakapokuwa wanakunywa maziwa kwa kuwa bado wanaendelea kukua faida na matokeo katika miili na ngozi zao watayaona.
“Licha ya kunywa vinywaji vingine vyenye sukari, bado wanahitaji kunywa maziwa kwa kuwa wanajenga miili yao tunataka kupelekea ujumbe kwa vijana.”
Sechonge amesema wameamua kumpa ubalozi Mbosso kwa kuwa anaweza kufikisha ujumbe kwa vijana pia ni mzazi mchanga.
“Tunataka kuongea na vijana wanywe maziwa lakini tunataka kuanza kuwafundisha watoto kunywa maziwa tumemchukua kwa kuwa tunataka kuongea na wazazi ambao wanataka kujenga familia sasa, pia tumegundua atakuwa balozi mzuri kwetu.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Fresh, Innocent Mushi amesema kampuni hiyo imeboresha bidhaa zake kwa sasa.
“Tanga Fresh itaendelea kuboresha bidhaa zake na huduma zake katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kuhakikisha tunaendelea kubakia kuwa chaguo namba moja la watumiaji wa bidhaa za maziwa Tanzania.” Amesema Mushi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *