Mbelgiji Simba Akesha Siku Mbili Akiwasoma Ihefu, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 5, 2020

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema ilibidi akeshe siku mbili akiwa anazisoma mbinu za Ihefu SC kabla ya kesho Jumapili kuvaana nao katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya kucheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.Sven ameeleza kuwa, aliamua kufanya hivyo kwa sababu Ihefu ni timu ngeni katika ligi na makocha wengi hawaifahamu akiwemo yeye, hivyo alitakiwa kuwasoma mapema na kujua atakwenda kukabiliana nao vipi.Akizungumza na Championi Jumamosi, Sven alisema mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao kwa sababu hakuna kitu kibaya kucheza na timu ngeni kwenye ligi kwa kuwa itaingia uwanjani ikihitaji kuzuia na kucheza kwa kushitukiza, huku akiweka bayana kuwa kukesha kwake akiisoma timu hiyo imemsaidia kugundua walau udhaifu wao.“Ilinibidi nilale usiku sana kwa siku mbili za mwanzo ambao tuliingia hapa Mbeya, Ihefu ni timu ngeni kwenye ligi na watu wengi hatujui inachezaje, kwa hiyo nilikuwa naisoma mbinu yao kwa siku zote mbili, walau sasa nimepata mwanga wa namna gani tunaenda kucheza nao.“Mchezo huu hautakuwa rahisi kw etu hata kidogo, siku zote timu ngeni kwenye ligi zinapocheza na timu kubwa, huingia na mbinu ya kujilinda zaidi na kushambulia kwa kushitukiza na sisi tupo tayari kwa hilo,” alisema Sven,

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema ilibidi akeshe siku mbili akiwa anazisoma mbinu za Ihefu SC kabla ya kesho Jumapili kuvaana nao katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya kucheza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Sven ameeleza kuwa, aliamua kufanya hivyo kwa sababu Ihefu ni timu ngeni katika ligi na makocha wengi hawaifahamu akiwemo yeye, hivyo alitakiwa kuwasoma mapema na kujua atakwenda kukabiliana nao vipi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Sven alisema mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao kwa sababu hakuna kitu kibaya kucheza na timu ngeni kwenye ligi kwa kuwa itaingia uwanjani ikihitaji kuzuia na kucheza kwa kushitukiza, huku akiweka bayana kuwa kukesha kwake akiisoma timu hiyo imemsaidia kugundua walau udhaifu wao.

“Ilinibidi nilale usiku sana kwa siku mbili za mwanzo ambao tuliingia hapa Mbeya, Ihefu ni timu ngeni kwenye ligi na watu wengi hatujui inachezaje, kwa hiyo nilikuwa naisoma mbinu yao kwa siku zote mbili, walau sasa nimepata mwanga wa namna gani tunaenda kucheza nao.

“Mchezo huu hautakuwa rahisi kw etu hata kidogo, siku zote timu ngeni kwenye ligi zinapocheza na timu kubwa, huingia na mbinu ya kujilinda zaidi na kushambulia kwa kushitukiza na sisi tupo tayari kwa hilo,” alisema Sven

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *