Maziwa makubwa ya Bonde la Ufa Kenya yanaendelea kufurika,

October 2, 2020

 

Maziwa mawili makubwa katika eneo la Bonde la ufa nchini Kenya yameshuhudia ongezeko la juu la viwango vya maji kwa miezi kadhaa sasa kufuatia mvua kubwa inayoendeleza kunyesha katika eneo hilo.

Lango kuu la kuingia mbuga ya kitaifa ya Nakuru limesombwa baada ya viwango vya maji kupanda. Kuna hofu maji katika maziwa mawili ya Baringo na Bogoria, ambayo moja ni ya maji ya chumvi yatachangayika.

Mafuriko hayo yamesababisha maelfu ya watu kuhama makwao baada ya nyumba na mashamba yao kusombwa na. Ukataji haramu wa miti umedaiwa kuchangia eneo hilo kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara.

Ukubwa wa maziwa hayo mawili umeongezeka karibu marambilina mamlaka katika eneo hilo imelazimika kutafuta njia mbadala ya kufika katika mbuga zinazopakana na hapo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *