Maxrioba: Mimi Meneja Tena wa Wema Tena Wala Mobeto

September 16, 2020

ALIYEWAHI kuwa meneja wa Hamisa Mobetto, Max Rioba ameweka wazi kuwa kwa sasa yeye sio meneja wa Hamisa Mobetto tena wala sio meneja wa Wema Sepetu ila anafanya nao kazi tu. Max amedokeza kuwa katika Tamthilia yake ya WE MEN wameanza mazungumzo na wasanii wa nje kama P Square kutoka Nigeria Casper Nyovest kutoka Afrika Kusini na Saut Soul kutoka Kenya ili waanza kufanya nao kazi kwenye Tamthilia hiyo. Lakini pia Max akiwa kama mtu wa karibu wa Wema Sepetu ametoa maoni yake kuhusu kinachoendelea kati ya wasanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu na Batuli kujibizana mitandaoni hadi kupeleka Batuli kumpost Wema na kuandika maneno ambayo yalionekana kutomfurahisha Wema, Max ametoa maoni yake na kusema kinachotakiwa ni heshima Batuli hakupaswa kuandika maneno kama yale kwa msanii mwenzake.,

ALIYEWAHI kuwa meneja wa Hamisa Mobetto, Max Rioba ameweka wazi kuwa kwa sasa yeye sio meneja wa Hamisa Mobetto tena wala sio meneja wa Wema Sepetu ila anafanya nao kazi tu.

 

Max amedokeza kuwa katika Tamthilia yake ya WE MEN wameanza mazungumzo na wasanii wa nje kama P Square kutoka Nigeria Casper Nyovest kutoka Afrika Kusini na Saut Soul kutoka Kenya ili waanza kufanya nao kazi kwenye Tamthilia hiyo.

 

Lakini pia Max akiwa kama mtu wa karibu wa Wema Sepetu ametoa maoni yake kuhusu kinachoendelea kati ya wasanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu na Batuli kujibizana mitandaoni hadi kupeleka Batuli kumpost Wema na kuandika maneno ambayo yalionekana kutomfurahisha Wema, Max ametoa maoni yake na kusema kinachotakiwa ni heshima Batuli hakupaswa kuandika maneno kama yale kwa msanii mwenzake.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *