Mavunde aanza kampeni rasmi, aahidi mikopo kwa Wanawake na Vijana, on September 6, 2020 at 10:15 am

September 6, 2020

CHAMA cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma kimezindua kampeni zake za Ubunge wa Jimbo hilo ambalo anagombea Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Anthony Mavunde kwa kipindi cha pili.Uzinduzi wa kampeni hizo ulikua wa kipekee kutokana na kuhudhuria na viongozi wa ndani na nje ya Dodoma, maelfu ya wananchi na wasanii mbalimbali wakiongozwa na mkali wa Bongo Fleva, Ben Pol.Akizungumza wakati wa kuomba kura, Mavunde amesema kwa miaka mitano aliyokua Mbunge ametekeleza kwa kiwango kikubwa ahadi zake ikiwemo kujenga Shule kwa kutumia nguvu zake nje ya fedha za serikali, kuchimba visima pamoja na kugawa vishkwambi kwa kila shule za serikali ili wanafunzi waweze kusoma kwa kisasa na kutumia teknolojia zaidi.Mavunde amesema miaka mitano ingine ataitumia kuboresha zaidi sekta ya elimu kwa kujenga shule zaidi, kugawa Kompyuta kwenye kila shule ya serikali, kutoa mikopo kwa vijana na wanawake pamoja na kuhakikisha analinda maslahi ya wananchi wake kwa kushirikiana na serikali.Ametumia nafasi hiyo kumuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli pamoja na madiwani wa kata 41 wanaotokana na chama hicho.” Rais wetu anatupenda sana, naombeni mumpigie kura nyingi za ndio Oktoba 28, mjitokeze kwa wingi mkaioneshe Dunia jinsi Dodoma inavyompenda Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyotufanyia.Miaka mitano tu Magufuli amehamishia Serikali yote Dodoma, ametujengea barabara za kisasa na kutufanya tuongoze kwa mtandao wa lami, ameboresha vituo vyetu vitatu vya afya, amejenga soko na stendi kubwa na kisasa, twendeni tukamshukuru Magufuli Oktoba 28 kwa kumpa kura nyingi hadi wapinzani waone aibu,” Amesema Mavunde.Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani na Mgombea Ubunge Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene amewaomba wananchi wa Dodoma kumchagua kwa wingi Rais Magufuli, Mavunde pamoja na madiwani wa CCM ili maendeleo yazidi kuja kwa wingi.” Msifanye makosa watu wa Dodoma, Mavunde amefanya makubwa, ile kero ya CDA siku hizi haipo kijana kaingia na bahati tu Dodoma imekua Jiji, nawahakikishia mkimchagua tena atafanya mambo mengi zaidi ya sasa,” Amesema Simbachawene.,

CHAMA cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma kimezindua kampeni zake za Ubunge wa Jimbo hilo ambalo anagombea Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Anthony Mavunde kwa kipindi cha pili.

Uzinduzi wa kampeni hizo ulikua wa kipekee kutokana na kuhudhuria na viongozi wa ndani na nje ya Dodoma, maelfu ya wananchi na wasanii mbalimbali wakiongozwa na mkali wa Bongo Fleva, Ben Pol.

Akizungumza wakati wa kuomba kura, Mavunde amesema kwa miaka mitano aliyokua Mbunge ametekeleza kwa kiwango kikubwa ahadi zake ikiwemo kujenga Shule kwa kutumia nguvu zake nje ya fedha za serikali, kuchimba visima pamoja na kugawa vishkwambi kwa kila shule za serikali ili wanafunzi waweze kusoma kwa kisasa na kutumia teknolojia zaidi.

Mavunde amesema miaka mitano ingine ataitumia kuboresha zaidi sekta ya elimu kwa kujenga shule zaidi, kugawa Kompyuta kwenye kila shule ya serikali, kutoa mikopo kwa vijana na wanawake pamoja na kuhakikisha analinda maslahi ya wananchi wake kwa kushirikiana na serikali.

Ametumia nafasi hiyo kumuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli pamoja na madiwani wa kata 41 wanaotokana na chama hicho.

” Rais wetu anatupenda sana, naombeni mumpigie kura nyingi za ndio Oktoba 28, mjitokeze kwa wingi mkaioneshe Dunia jinsi Dodoma inavyompenda Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyotufanyia.

Miaka mitano tu Magufuli amehamishia Serikali yote Dodoma, ametujengea barabara za kisasa na kutufanya tuongoze kwa mtandao wa lami, ameboresha vituo vyetu vitatu vya afya, amejenga soko na stendi kubwa na kisasa, twendeni tukamshukuru Magufuli Oktoba 28 kwa kumpa kura nyingi hadi wapinzani waone aibu,” Amesema Mavunde.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani na Mgombea Ubunge Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene amewaomba wananchi wa Dodoma kumchagua kwa wingi Rais Magufuli, Mavunde pamoja na madiwani wa CCM ili maendeleo yazidi kuja kwa wingi.

” Msifanye makosa watu wa Dodoma, Mavunde amefanya makubwa, ile kero ya CDA siku hizi haipo kijana kaingia na bahati tu Dodoma imekua Jiji, nawahakikishia mkimchagua tena atafanya mambo mengi zaidi ya sasa,” Amesema Simbachawene.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *