Mastaa Hawa ni Chui na Paka

September 16, 2020

KWENYE muziki, ni kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida, kuna baadhi ya wasanii wao wamejikuta kutokana na sababu zao, hawapikiki chungu kimoja. Wao ni maadui mwanzo mwisho, ni kama chui na paka.Twende tukawatazame mmoja baada ya mwingine:DIAMOND & KIBAHawa bifu lao ni la muda mrefu sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na mwenzake Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ na ndilo bifu linalosemwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Bifu la wawili hawa, lilianza kama utani baada ya kusemekana Diamond au Mondi, ndiye aliyemkera mwenzake baada ya kumfuta kwenye Wimbo wa Lala Salama. Mara kadhaa Mondi ameonekana kuwa tayari kupatana na hasimu wake huyo, lakini Kiba amekuwa akichomoa vibaya kuhusu suala hilo.AKA NA CASSPER NYOVESTWakati hapa Bongo tunawaangalia Ali Kiba na Diamond, kule Afrika Kusini kuna Rapper Kiernan Jarryd Forbes ‘AKA na Refiloe Maele Phoolo ‘Cassper Nyovest’, wawili hawa walikuwa na bifu la ukweli na siyo la kutengenezwa na mashabiki, ambapo unaambiwa AKA ndiye alianza kum-diss Nyovest katika wimbo wake wa Composure.Cassper alikiri kwamba, wimbo wa AKA umemuumiza  sana na yeye alijibu mashambulizi kwa kuachia ngoma mbili kwa mpigo, zilizomdiss AKA, ambazo ni Back to Back na Ashes to Ashes. Hakuishia hapo, Nyovest tena akaachia diss track inayojulikana kwa jina la Dust to Dust, ambayo ilimuumiza vilivyo AKA na kuapa kutokuelewana na Nyovest.YEMI ALADE NA TIWA SAVAGEAwali, Tiwatope Savage ‘Tiwa Savage’ na Yemi Eberechi Alade ‘Yemi Alade’ wamekuwa wakihusishwa kuwa kwenye bifu kwa muda mrefu, lakini kwa upande wao hawakuwahi kukiri popote kuhusiana na tuhuma hizo.Desemba 21, 2018 bifu hilo limeonekana kuwekwa wazi baada ya Yemi Alade kumtupia dongo Tiwa juu ya muonekano wake na kusema kuwa, amekuwa akijibinua kwenye picha ili kupata muonekano mzuri hususan eneo la makalio, ili yaonekane makubwa.Yemi Alade aliandika; “Acha kuongeza makalio yako kwenye picha, unajijua kuwa upo kama I, jikubali ulivyo Ahh ahh, unawadanganya mashabiki wako juu na chini.”Kwa upande wake Tiwa, alionekana kupokea dongo hilo kutoka kwa Yemi Alade na kumjibu kupitia page yake ya Twitter na kusema kuwa, hayuko kwenye vita ya makalio na hatokaa kumhukumu mwanamke yeyote hata awe ana vitu ‘fake’. Hadi kufikia hatua hii, hakuna ‘anayem-follow’ mwenzake katika mitandao ya kijamii.Mashabiki wa wanamuziki hao, wametoa maoni yao kuhusu bifu lao na kusema kuwa, wanatakiwa wasuluhishwe kwa sababu ni wasanii wakubwa na ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wadogo wa kike, na inaonekana wakifanya shoo ya pamoja itapendeza zaidi machoni mwa mashabiki wa muziki wao.Makala: Khadija bakari,

KWENYE muziki, ni kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida, kuna baadhi ya wasanii wao wamejikuta kutokana na sababu zao, hawapikiki chungu kimoja. Wao ni maadui mwanzo mwisho, ni kama chui na paka.

Twende tukawatazame mmoja baada ya mwingine:

DIAMOND & KIBA

Hawa bifu lao ni la muda mrefu sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na mwenzake Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ na ndilo bifu linalosemwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Bifu la wawili hawa, lilianza kama utani baada ya kusemekana Diamond au Mondi, ndiye aliyemkera mwenzake baada ya kumfuta kwenye Wimbo wa Lala Salama. Mara kadhaa Mondi ameonekana kuwa tayari kupatana na hasimu wake huyo, lakini Kiba amekuwa akichomoa vibaya kuhusu suala hilo.

AKA NA CASSPER NYOVEST

Wakati hapa Bongo tunawaangalia Ali Kiba na Diamond, kule Afrika Kusini kuna Rapper Kiernan Jarryd Forbes ‘AKA na Refiloe Maele Phoolo ‘Cassper Nyovest’, wawili hawa walikuwa na bifu la ukweli na siyo la kutengenezwa na mashabiki, ambapo unaambiwa AKA ndiye alianza kum-diss Nyovest katika wimbo wake wa Composure.

Cassper alikiri kwamba, wimbo wa AKA umemuumiza  sana na yeye alijibu mashambulizi kwa kuachia ngoma mbili kwa mpigo, zilizomdiss AKA, ambazo ni Back to Back na Ashes to Ashes. Hakuishia hapo, Nyovest tena akaachia diss track inayojulikana kwa jina la Dust to Dust, ambayo ilimuumiza vilivyo AKA na kuapa kutokuelewana na Nyovest.

YEMI ALADE NA TIWA SAVAGE

Awali, Tiwatope Savage ‘Tiwa Savage’ na Yemi Eberechi Alade ‘Yemi Alade’ wamekuwa wakihusishwa kuwa kwenye bifu kwa muda mrefu, lakini kwa upande wao hawakuwahi kukiri popote kuhusiana na tuhuma hizo.

Desemba 21, 2018 bifu hilo limeonekana kuwekwa wazi baada ya Yemi Alade kumtupia dongo Tiwa juu ya muonekano wake na kusema kuwa, amekuwa akijibinua kwenye picha ili kupata muonekano mzuri hususan eneo la makalio, ili yaonekane makubwa.

Yemi Alade aliandika; “Acha kuongeza makalio yako kwenye picha, unajijua kuwa upo kama I, jikubali ulivyo Ahh ahh, unawadanganya mashabiki wako juu na chini.”

Kwa upande wake Tiwa, alionekana kupokea dongo hilo kutoka kwa Yemi Alade na kumjibu kupitia page yake ya Twitter na kusema kuwa, hayuko kwenye vita ya makalio na hatokaa kumhukumu mwanamke yeyote hata awe ana vitu ‘fake’. Hadi kufikia hatua hii, hakuna ‘anayem-follow’ mwenzake katika mitandao ya kijamii.

Mashabiki wa wanamuziki hao, wametoa maoni yao kuhusu bifu lao na kusema kuwa, wanatakiwa wasuluhishwe kwa sababu ni wasanii wakubwa na ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wadogo wa kike, na inaonekana wakifanya shoo ya pamoja itapendeza zaidi machoni mwa mashabiki wa muziki wao.

Makala: Khadija bakari

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *