Mashirika ya Umoja wa Mataifa yataka Ulaya kuchukua wakimbizi zaidi kutoka Ugiriki, on September 15, 2020 at 6:00 pm

September 15, 2020

 Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema leo kuwa mataifa ya Ulaya yanahitaji kuwachukua wahamiaji zaidi kutoka Lesbos pamoja na makambi mengine yaliyojaa watu katika visiwa vingine vya Ugiriki. Mkuu wa shirika la kimataifa la kuwahudumia wahamiaji IOM Antonio Vitorino amesema katika taarifa kuwa inahitajika nia thabiti ya kuwachukua wakimbizi katika nyakati hizi ngumu wakati Umoja wa Ulaya unatayarisha mfumo ambao unaweza kufanya kazi chini ya wajibu wa kugawana majukumu. Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR nchini Ugiriki Philippe Leclerc, amesema kuwa idadi ya watu katika vituo vya kuwahifadhia wakimbizi katika visiwa vya Ugiriki wanapaswa kupunguzwa na mazingira ya kuishi ni lazima yawe bora.,

 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema leo kuwa mataifa ya Ulaya yanahitaji kuwachukua wahamiaji zaidi kutoka Lesbos pamoja na makambi mengine yaliyojaa watu katika visiwa vingine vya Ugiriki. 

Mkuu wa shirika la kimataifa la kuwahudumia wahamiaji IOM Antonio Vitorino amesema katika taarifa kuwa inahitajika nia thabiti ya kuwachukua wakimbizi katika nyakati hizi ngumu wakati Umoja wa Ulaya unatayarisha mfumo ambao unaweza kufanya kazi chini ya wajibu wa kugawana majukumu. 

Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR nchini Ugiriki Philippe Leclerc, amesema kuwa idadi ya watu katika vituo vya kuwahifadhia wakimbizi katika visiwa vya Ugiriki wanapaswa kupunguzwa na mazingira ya kuishi ni lazima yawe bora.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *