Mashabiki watalazimika kulipa ili kutazama mechi ambazo hazitaoneshwa kwenye televisheni

October 9, 2020

Dakika 4 zilizopita

Mpira wa miguu umekuwa ukichezwa bila kuwepo mashabiki uwanjani kutokana na marufuku ya kutotoka nje

Mechi za ligi ya primia ambazo hazijachaguliwa kutangazwa kwenye televisheni mwezi Oktoba zitashuhudiwa na mashabiki baada ya kuzilipia.

Mechi tano hazijachaguliwa kuoneshwa mubashara lakini watu wanaweza kulipia kiasi cha pauni 14.95 ili kuziangalia.

Klabu zimekubaliana na suluhisho hilo la muda ili kuruhusu mashabiki kuendelea kuangalia timu zao moja kwa moja.

Ligi ya Primia imesema yenyewe na klabu zake zitaendelea kuwajibika kuwarejesha mashabiki wake haraka iwezekanavyo “.

Kandanda imekuwa ikichezwa bila mashabiki kuwepo uwanjani tangu marufuku kutokana na virusi vya corona ilipowekwa.

Beki wa zamani wa kulia wa Manchester United Gary Neville, ambaye sasa ni mchambuzi katika televisheni alisema katika mtandao wa kijamii kuwa hatua iliyochukuliwa na ligi ya primia ni mbaya sana.

Premier League na serikali ya Uingereza ilikuwa na matumaini ya kurejesha mashabiki Oktoba Mosi lakini mipango hiyo imebadilika kutokana na ongezeko la maambukizi ya corona.

Katika taarifa kutoka kwa wadau wa soka wametaka warusha matangazo wafikirie kuhusu suala la kupunguza bei.

“Tangazo la leo linaonesha kuwa nguvu ya mashabiki inafanya kazi ,” FSA imeeleza.

“Mwanzoni mwa msimu ligi ya primia na watangazaji wake walipanga kuacha mechi ziendelee bila ya mashabiki kuona lakini sasa msukumo wa kampeni za mashabiki umezaa matunda na mechi hizo kuweza kuonekana.

“klabu nyingi za ligi ya primia zilichukua tayari pesa za mashabiki ambao walinunua tiketi na hawawezi kwenda kuona, hivyo tumewataka kurejesha fedha hizo kwa mashabiki mapema iwezekanavyo.

“Tumesikia tayari kutoka kwa mashabiki wengi na wanachama wa FSA ambao wanahofia kuhusu suala la kulipa £15 kwa kila mechi na hivyo inabidi wafikiriwe katika malipo ya mechi hizi.”

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *