Mashabiki wa Yanga huenda wasiamini…TFF Wamtabulisha Rasmi Morrison Kama Mchezaji wa Simba, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 3, 2020

Mashabiki wa Yanga huenda wasiamini, lakini ukweli ni kwamba winga wao nyota aliyetangazwa kuwa miongoni mwa wachezaji 28 wa kikosi chao kwa msimu ujao, Bernard Morrison ndio basi tena baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtambulisha rasmi kama mchezaji wa Simba.#Morrison aliyekuwa na mvutano na mabosi wake hao wa zamani, alitajwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi kama mchezaji wa Yanga, akiwa jijini Arusha kukinukisha kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ya timu yake mpya ya Simba iliyoishinda Namungo kwa mabao 2-0.Lakini mashabiki wakiwa bado hawaamini kama nyota huyo aliyewapa raha msimu uiliopita kwa kuwatungua Simba katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara, atasalia kikosini mwao, katika orodha ya usajili mpya ya TFF kwa msimu ujao jina lake limatokezea Simba kuonyesha ni mali yao rasmi sasa.Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo amefichua kilichomfanya Morrison awe kwenye orodha ya Simba badala ya ile ya Yanga ni kwa kuzingatia maamuzi ya Kamati yo ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji iliyomtambulisha kama mchezaji huru baada ya kusikiliza kesi iliyomhusisha Mghana huyo na Yanga.,

Mashabiki wa Yanga huenda wasiamini, lakini ukweli ni kwamba winga wao nyota aliyetangazwa kuwa miongoni mwa wachezaji 28 wa kikosi chao kwa msimu ujao, Bernard Morrison ndio basi tena baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtambulisha rasmi kama mchezaji wa Simba.

#Morrison aliyekuwa na mvutano na mabosi wake hao wa zamani, alitajwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi kama mchezaji wa Yanga, akiwa jijini Arusha kukinukisha kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ya timu yake mpya ya Simba iliyoishinda Namungo kwa mabao 2-0.

Lakini mashabiki wakiwa bado hawaamini kama nyota huyo aliyewapa raha msimu uiliopita kwa kuwatungua Simba katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara, atasalia kikosini mwao, katika orodha ya usajili mpya ya TFF kwa msimu ujao jina lake limatokezea Simba kuonyesha ni mali yao rasmi sasa.

Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo amefichua kilichomfanya Morrison awe kwenye orodha ya Simba badala ya ile ya Yanga ni kwa kuzingatia maamuzi ya Kamati yo ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji iliyomtambulisha kama mchezaji huru baada ya kusikiliza kesi iliyomhusisha Mghana huyo na Yanga.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *