Mashabiki: Mondi, Zuchu Waoane Tu Yaishe

September 17, 2020

BORA waoane tu yaishe! Ndivyo wanavyosema mamilioni ya mashabiki wa mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’ wakimtaka jamaa huyo afunge ndoa na msanii wake, Zuhura Othman ‘Zuchu’.LITAWACHOMA/CHECHEKauli hizo zinasukumwa na nyimbo mbili walizoachia wawili hao kwa mpigo, wikiendi iliyopita za Litawachoma na Cheche, ambazo zinapishana katika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye ‘platforms’ (mitandao mbalimbali ya kusikiliza, kutazama na kuuza muziki) barani Afrika kama Apple Store, Itune, Spotify, Dezeer, Audiomack, Soundcloud, YouTube, Amazon, Mdundo, Boomplay na nyingine nyingiMashairi ya nyimbo hizo, yanagusa hisia za wengi, kiasi cha kuwateka na kuwapumbaza mashabiki wao, ambao sasa wanaunga mkono zile stori za Diamond au Mondi na Zuchu kuwa mbioni kufunga ndoa.Mondi ameshatangaza siku ya Oktoba 2, mwaka huu kuwa ndiyo siku atakayofunga ndoa, lakini kuhusu atamuoa nani, hakuweka hadharani.WATEKA HISIASasa, Mondi na Zuchu wameteka hisia za wapenda burudani ndani na nje ya Bongo, ambao wamewanyooshea mikono na kuona bora waoane.Kila anayesikiliza nyimbo hizo, anasema zimebeba ujumbe mzito wa mahaba, hasa huo wa Litawachoma ambao mashairi yake yanaonesha kuna watu hawapendi kuwaona pamoja, lakini kupitia wimbo huo, ujumbe umewafikia.Ghafla tu, sasa gumzo kubwa kwa mara nyingine ni Mondi na Zuchu kwamba, kwa namna walivyopita kwenye nyimbo hizo, wanafaana kuwa kapo (wapenzi) wa kudumu.mahaba Kama YoteKwenye nyimbo hizo, Mondi na Zuchu wanajibizana kwa mahaba kama yote, hivyo wanafaa kuwa mke na mume au wanandoa.KWENYE YOUTUBENdani ya saa kadhaa tangu nyimbo hizo ziachiwe, zilianza kukimbiza kwenye Mtandao wa YouTube, ambapo ndani ya muda mfupi, zilikuwa na wasikilizaji zaidi ya laki 5 kwa kila moja.Kwa upande wa mashabiki, walizisifia na kuzikubali kazi hizo kutoka kwa bosi huyo wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) na msanii wake, Zuchu.“Hizi ngoma ni kali sana. Sijawahi kuona tangu nizaliwe. Queen of Bongo Fleva; Zuchu na King of Bongo Fleva; Diamond Platnumz.“Zuchu, Diamond Platnumz na WCB Mungu yupo na hakuna wa kuwatenganisha au kuwashusha.“Kiukweli lazima Watanzania tujivunie kapo hii (Zuchu na Mondi).“Diamond na Zuchu toeni nyimbo nyingi kama hizi mnapendezea sana.“Hawa ndiyo Diamond na Zuchu, bado tunasubiri kuhalalisha tu ndoa maana bora waoane, maneno mengi yaishe.“Jamani Diamond na Zuchu mambo ni faya,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki kwenye audio za nyimbo hizo kwenye Mtandao wa YouTube.Kwa mujibu wa wachambuzi wa nyimbo hizo, kwenye video zake kunategemewa kuwa na scenes (vipande vya video) nyingi za mahaba, kwani wamekuwa wakipendezeana mno kwenye kipengele hicho.“Kama kweli wataamua kuigiza video za nyimbo hizi za kimahaba, basi itakuwa ni biashara kubwa mno,” alisema mmoja wa wadau na kuongeza;“Hakuna kinachosubiriwa kama video za nyimbo hizi, kwani Zuchu anatarajiwa kujiachia kimahaba na kumvua Mondi ubosi na kumchukulia kama mpenzi wake.”ZITAMUWEKA ZUCHU JUUWachambuzi wengine wanasema kuwa, mbali na watu kufurahia kuona mahaba ya wawili hao, lakini nyimbo hizo zitamuweka Zuchu juu, kwani Mondi ni msanii mkubwa ndani na nje ya Bongo, hivyo zitampeleka mbali zaidi.MONDI NA ZUCHUVuguvugu la Mondi kutakiwa kumuoa Zuchu, lilianza muda mfupi tu baada ya Aprili 8, mwaka huu, pale mrembo huyo aliposainiwa kwenye Lebo ya WCB iliyo chini ya Mondi.Baada ya hapo, wawili hao wakawa wanapostiana kwenye mitandao ya kijamii na familia ya Mondi kumsifia Zuchu kwa kufungua ukurasa mpya wa maisha ndani ya familia yao.Yote hayo yalikuja siku chache baada ya Mondi kutamka kuwa kwa sasa hahitaji tena maisha ya kurukaruka na wanawake na kwamba, jamii ikimsikia, basi atakuwa ameoa.Katika hali inayoonesha kuwa mashabiki wa Mondi wanaipenda kapo yake na Zuchu, mara kadhaa wamekuwa wakishabiki,

BORA waoane tu yaishe! Ndivyo wanavyosema mamilioni ya mashabiki wa mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’ wakimtaka jamaa huyo afunge ndoa na msanii wake, Zuhura Othman ‘Zuchu’.

LITAWACHOMA/CHECHE

Kauli hizo zinasukumwa na nyimbo mbili walizoachia wawili hao kwa mpigo, wikiendi iliyopita za Litawachoma na Cheche, ambazo zinapishana katika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye ‘platforms’ (mitandao mbalimbali ya kusikiliza, kutazama na kuuza muziki) barani Afrika kama Apple Store, Itune, Spotify, Dezeer, Audiomack, Soundcloud, YouTube, Amazon, Mdundo, Boomplay na nyingine nyingi

Mashairi ya nyimbo hizo, yanagusa hisia za wengi, kiasi cha kuwateka na kuwapumbaza mashabiki wao, ambao sasa wanaunga mkono zile stori za Diamond au Mondi na Zuchu kuwa mbioni kufunga ndoa.

Mondi ameshatangaza siku ya Oktoba 2, mwaka huu kuwa ndiyo siku atakayofunga ndoa, lakini kuhusu atamuoa nani, hakuweka hadharani.

WATEKA HISIA

Sasa, Mondi na Zuchu wameteka hisia za wapenda burudani ndani na nje ya Bongo, ambao wamewanyooshea mikono na kuona bora waoane.

Kila anayesikiliza nyimbo hizo, anasema zimebeba ujumbe mzito wa mahaba, hasa huo wa Litawachoma ambao mashairi yake yanaonesha kuna watu hawapendi kuwaona pamoja, lakini kupitia wimbo huo, ujumbe umewafikia.

Ghafla tu, sasa gumzo kubwa kwa mara nyingine ni Mondi na Zuchu kwamba, kwa namna walivyopita kwenye nyimbo hizo, wanafaana kuwa kapo (wapenzi) wa kudumu.mahaba Kama YoteKwenye nyimbo hizo, Mondi na Zuchu wanajibizana kwa mahaba kama yote, hivyo wanafaa kuwa mke na mume au wanandoa.

KWENYE YOUTUBE

Ndani ya saa kadhaa tangu nyimbo hizo ziachiwe, zilianza kukimbiza kwenye Mtandao wa YouTube, ambapo ndani ya muda mfupi, zilikuwa na wasikilizaji zaidi ya laki 5 kwa kila moja.

Kwa upande wa mashabiki, walizisifia na kuzikubali kazi hizo kutoka kwa bosi huyo wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) na msanii wake, Zuchu.“Hizi ngoma ni kali sana. Sijawahi kuona tangu nizaliwe. Queen of Bongo Fleva; Zuchu na King of Bongo Fleva; Diamond Platnumz.

“Zuchu, Diamond Platnumz na WCB Mungu yupo na hakuna wa kuwatenganisha au kuwashusha.“Kiukweli lazima Watanzania tujivunie kapo hii (Zuchu na Mondi).

“Diamond na Zuchu toeni nyimbo nyingi kama hizi mnapendezea sana.“Hawa ndiyo Diamond na Zuchu, bado tunasubiri kuhalalisha tu ndoa maana bora waoane, maneno mengi yaishe.“Jamani Diamond na Zuchu mambo ni faya,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki kwenye audio za nyimbo hizo kwenye Mtandao wa YouTube.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa nyimbo hizo, kwenye video zake kunategemewa kuwa na scenes (vipande vya video) nyingi za mahaba, kwani wamekuwa wakipendezeana mno kwenye kipengele hicho.

“Kama kweli wataamua kuigiza video za nyimbo hizi za kimahaba, basi itakuwa ni biashara kubwa mno,” alisema mmoja wa wadau na kuongeza;“Hakuna kinachosubiriwa kama video za nyimbo hizi, kwani Zuchu anatarajiwa kujiachia kimahaba na kumvua Mondi ubosi na kumchukulia kama mpenzi wake.”

ZITAMUWEKA ZUCHU JUU

Wachambuzi wengine wanasema kuwa, mbali na watu kufurahia kuona mahaba ya wawili hao, lakini nyimbo hizo zitamuweka Zuchu juu, kwani Mondi ni msanii mkubwa ndani na nje ya Bongo, hivyo zitampeleka mbali zaidi.

MONDI NA ZUCHU

Vuguvugu la Mondi kutakiwa kumuoa Zuchu, lilianza muda mfupi tu baada ya Aprili 8, mwaka huu, pale mrembo huyo aliposainiwa kwenye Lebo ya WCB iliyo chini ya Mondi.

Baada ya hapo, wawili hao wakawa wanapostiana kwenye mitandao ya kijamii na familia ya Mondi kumsifia Zuchu kwa kufungua ukurasa mpya wa maisha ndani ya familia yao.

Yote hayo yalikuja siku chache baada ya Mondi kutamka kuwa kwa sasa hahitaji tena maisha ya kurukaruka na wanawake na kwamba, jamii ikimsikia, basi atakuwa ameoa.

Katika hali inayoonesha kuwa mashabiki wa Mondi wanaipenda kapo yake na Zuchu, mara kadhaa wamekuwa wakishabiki

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *