Martha Umbura amuombea kura Magufuli kwa wanawake Manyara,

October 2, 2020

Na John Walter-Manyara

MGOMBEA Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Manyara  kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Martha Umbura  amewaomba wakina mama mkoani humo kupiga kura za kishindo kwa Rais Magufuli na Wagombea wote wa Chama hicho.

Umbura amesema kuwa  kwa mengi yaliyofanywa Mkoa wa Manyara na  Rais John  Magufuli, zawadi pekee ya kumpa ni kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.  

Amewataka wananchi wote Mkoa wa Manyara  kuhakikisha wanapiga kura zote kwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi.

Umbura amesema haoni sababu ya Dk. Magufuli kutompa miaka mingine mitano, kwani ameonesha dhahiri  kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita nia yake ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania kupata huduma bora kwenye afaya, Elimu na kuboresha Miundombinu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *