Mariam Ditopile ataja faida ya Ndege za Rais Magufuli, “Zinakuza uchumi wetu”,

October 2, 2020

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile ameshiriki kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ambapo pamoja na kumnadi yeye na Mgombea Urais, Dk John Magufuli katika kata ya Hombolo pia ameeleza namna serikali ya Rais Magufuli ilivyofanikiwa kwenye sekta ya usafiri wa anga kabla ya hapo alianzia Kata ya Ikoa Jimbo la Chamwino kwenye vikao vya ndani.

” Dk Magufuli amefanikiwa kufufua shirika letu la Ndege tena kwa kutumia fedha zetu wenyewe kanunua Ndege 11, 2015 wapinzani kwenye ilani yao walisema katika kuboresha miundombinu watafufua shirika la ndege leo Magufuli ametekeleza kwa kishindo inauma, hawa ni wazalendo? Au wakwamishaji wa maendeleo yetu.

Serikali ya Magufuli haijanunua tu Ndege imeboresha viwanja vya ndege kikiwemo chetu cha Dodoma ambavyo vinaenda kuwa na hadhi kubwa, lakini pia hapa Dodoma Rais Magufuli ameshatoa fedha kiwanja kingine kikubwa kinajengwa, yote haya ni kuhakikisha tunakuza uchumi wetu kupitia sekta ya anga na kuchochea watalii kuja.

Ndege ni kichocheo cha uchumi hasa Utalii, ujio wa Ndege zetu pia zimechangia wingi wa watalii kuja Nchini maana sasa gharama zimepungua, hivyo lazima tuangalie namna watalii watavutiwa kwetu kuja kwa gharama nafuu, kwa kuleta ndege hizi gharama zimeshuka zamani watalii na tumeongeza mapato ya sekta ya utalii kwa zaidi ya asilimia   17.6 na fedha zinazopatikana ndizo zinajenga vituo vya afya, miundombinu na kuchangia elimu bure,” Amesema Ditopile.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *