Marekani yaomba Rwanda ‘kutoa mazingira ya kiutu’ kwa Rusesabagina, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 3, 2020 at 10:00 am

September 3, 2020

Marekani inatarajia serikali ya Rwanda “itatoa mazingira ya kibinadamu” kwa Paul Rusesabagina, shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda ”aliyekamatwa” na kupelekwa Rwanda.Naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Tibor Nagy amesema amekutana na Matilde Mukantabana nchini Marekani, kujadili suala la kukamatwa kwa bwana Rusesabagina.Rusesabagina,66, mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda amabaye anaishi ughaibuni aliangaziwa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.Alisimamishwakwa muda mfupi mbele ya wanahabari mjini Kigali siku ya Jumatatu.Maafisa hawakuelezea mazingira ya kukamatwa, lakini walisema alikamatwa kupitia kibali cha kimataifa kwa kuongoza “vuguvugu la kigaidi”.“Marekani inatarajia serikali ya Rwanda itatoa mazingira ya kiutu, kwa kuzingatia utawala wa sheria, kwa kuendesha machakato wa kisheria ulio wazi na usio na upendelea dhidi ya bwanaRusesabagina” Bwna Nagy aliandika katika kwenye Twitter yake baada ya kukutana nabalozi wa Rwanda.Bwana Rusesabagina, Mnyarwanda mwenye uraia wa Ubelgiji na makazi ya kudumu ya kiushi nchini Marekani alikuwa amesafiri kutoka San Antonio, Texas kwenda Dubai Alhamisi iliyopita,familia na chama chake kiliambia BBC.”Tunaamini alitekwa nyara kwasababu hawezi kuenda Rwanda kwa hiari yake.” Binti yake aliambia BBC.Serikali ya Rwanda haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai ya kutekwa kwake.,

Marekani inatarajia serikali ya Rwanda “itatoa mazingira ya kibinadamu” kwa Paul Rusesabagina, shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda ”aliyekamatwa” na kupelekwa Rwanda.

Naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Tibor Nagy amesema amekutana na Matilde Mukantabana nchini Marekani, kujadili suala la kukamatwa kwa bwana Rusesabagina.

Rusesabagina,66, mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda amabaye anaishi ughaibuni aliangaziwa katika filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Alisimamishwakwa muda mfupi mbele ya wanahabari mjini Kigali siku ya Jumatatu.

Maafisa hawakuelezea mazingira ya kukamatwa, lakini walisema alikamatwa kupitia kibali cha kimataifa kwa kuongoza “vuguvugu la kigaidi”.

“Marekani inatarajia serikali ya Rwanda itatoa mazingira ya kiutu, kwa kuzingatia utawala wa sheria, kwa kuendesha machakato wa kisheria ulio wazi na usio na upendelea dhidi ya bwanaRusesabagina” Bwna Nagy aliandika katika kwenye Twitter yake baada ya kukutana nabalozi wa Rwanda.

Bwana Rusesabagina, Mnyarwanda mwenye uraia wa Ubelgiji na makazi ya kudumu ya kiushi nchini Marekani alikuwa amesafiri kutoka San Antonio, Texas kwenda Dubai Alhamisi iliyopita,familia na chama chake kiliambia BBC.

“Tunaamini alitekwa nyara kwasababu hawezi kuenda Rwanda kwa hiari yake.” Binti yake aliambia BBC.

Serikali ya Rwanda haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai ya kutekwa kwake.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *