Marekani, Urusi kufanya mazungumzo ya silaha za nyuklia nchini Finland,

October 5, 2020

 

Marekani na Urusi zitaandaa awamu nyingine ya mazungumzo ya uthibiti wa silaha za nyuklia katika mji wa Helsinki nchini Finland hii leo kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika nchini Austria wakati wa majira ya kiangazi. 

Taarifa hiyo imetangazwa na Ofisi ya rais wa Finland Sauli Niinisto. Katika taarifa jana jioni, ofisi hiyo imesema kuwa awamu ya mazungumzo kuhusu mpango wa uthabiti na silaha za nyuklia kati ya Marekani na Urusi yaliyoanza mjini Vienna nchini Austria yataendelea leo nchini humo.

Ofisi hiyo imeendelea kusema kuwa wajumbe wa mazungumzo hayo kutoka mataifa hayo mawili walikutana katika miaka iliyopita nchini humo mnamo mwaka 2017 na kuongeza kuwa rais Niinisto atakutana nao baada ya mazungumzo hayo. 

Wajumbe hao ni balozi Marshall Billingslea wa Marekani na naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Ryabkov. 

Mazungumzo hayo yanalenga kupatikana kwa mkataba mpya utakaochukuwa nafasi ya mkataba ulioko sasa kwa jina NEW start ambao muda wake unafika mwisho mnamo mwezi Februari huu ukiwa mkataba wa mwisho unaodhibiti silaha za mataifa hayo mawili makubwa yenye silaha za nyuklia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *