Marekani na Israel hazitaki uchaguzi ufanyike Palestina,

October 4, 2020

Saib Ureykat, Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO), amesema kuwa Marekani na Israeli hawataki uchaguzi nchini Palestina.

Ureykat ametoa taarifa hiyo kupitia kituo cha redio cha “Sauti ya Palestina”, na kusema kuwa,

“Marekani na Israeli hawataki uchaguzi nchini Palestina kwa sababu hawataki kupingwa kwa Israel kukalia kimabavu ardhi ya Palestina.Washington na Tel Aviv hazitaki uhuru wa watu wetu. Wanaendelea na shughuli zao ambazo zinapingana na uhalali wa sheria za kimataifa.”

Akisisitiza kuwa vikundi vya Wapalestina vitafanikiwa kufikia umoja wa kitaifa licha ya vitisho na changamoto kutoka Marekani na Israeli, Ureykat amesema kuwa utawala utafanya uamuzi wa kuamua tarehe ya uchaguzi.

Ureykat amesema kuwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaendelea na mipango yake ya kuteka ardhi ya Wapalestina, licha ya madai ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Ahmed Abu Gayt, kwamba ameachana na harakati hizo.

Ureykat pia ameongeza kwa kusema kuwa hali ya makubaliano yaliyotiliwa saini kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu itasababisha machafuko na umwagaji damu katika ukanda huo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *