Marekani kupiga marufuku TikTok na WeChat

September 18, 2020

 TikTok na WeChat zitapigwa marufuku nchini Marekani kuanzia Jumapili, endapo Rais Donald Trump atakubali kutekeleza mkataba wa dakika za mwisho.Idara ya biashara ya imesema itawazuia watu nchini Marekani kupakua progamu hizo kupitia mtandao wowote.Utawala wa Trump unasema kampuni zinazomiliki mitandao hiyo ni tishio kwa usalama wa taifa na kwamba huenda ikwasilisha maelezo ya watumiaji wake kwa China.Lakini China na kampuni hizo zote mbili zimepinga madai hayo.WeChat itafungwa rasmi nchini Marekani siku ya Jumapili, lakini watu wataweza kutumia TikTok hadi tarehe 12 Novemba, wakati ambapo pia huenda ikafungwa.Ikiwa mpango wa ushirikiano kati ya kampuni ya teknolojia ya Marekani, Oracle na mwenyeji wa TikTok ByteDance utakubaliwa na kuidhinishwa na Rais Trump, programu hiyo huenda isipigwe marufuku.Haijabainika ikiwa bwana Trump ataidhinisha mpango huo, lakini anatarajiwa kutathmini hatua hiyo kabla ya siku ya Jumapili. Amri ya marufuku kutoka Idara ya Biashara inafuata amri ya rais iliyotiwa saini mwezi Agosti ambayo iliipatia biashara nchi Marekani siku 45 kuacha kufanya kazi na kampuni hizo mbili za China.”Kulingana na maelekezo ya rais, tumechukua hatua ya kudhibiti ulaghai wa China dhidi ya kukusanya taarifa binafsi ya watu wa Marekani,” Wiziri ya biashara Wilbur Ross alisema katika taarifa.Wizara hiyo ilikubali hofu ya kiusalama inayohusishwa na mitandao ya WeChat na TikTok haifanani lakini ilisema kwamba kila moja ilikusanya “maelezo mengi kutoka kwa watumiaji wa huduma yao, ikiwa ni pamoja na, mahali wanapoishi, mfumo wamawasiliano wanaotumia na na historia ya vitu wanavyotafuta mtandaoni”.Maafisa Marekani na wanasiasa wameonesha wasiwasi wao kuhusu data inayokusanywa na kampuni ya ByteDance kupitia programu ya TikTok kwamba huenda ikakabidhiwa serikali ya China.Nchini China, TikTok inatoa huduma sawa na hiyo lakini kupitia toleo jinginge la programu ya China inayofahamika kama Douyin.Pia inasema data ya watumiaji wote wa Marekani inahifadhiwa Marekani huku chelezo cha programu hiyo ikiwa Singapore.Wiki hii, kampuni ya TikTok iliwaambia watumiaji wake na wadhibiti kwamba huenda ikawa na uwazi wa hali ya juu ikiwemo kuruhusu kupitiwa tena kwa mfumo huo.”Hatuko kisiasa, haturuhusu matangazo ya kisiasa na hatuna ajenda yoyote – lengo letu kuu ni kuendelea kusisimua, kuwa mtandao ambao kila mmoja ataufurahia,” amesema Mkurugenzi mtendaji wa TikTok, Kevin Mayer, wiki hii.”TikTok imekuwa mlengwa mkuu, lakini sisi sio adui.”Programu hiyo imepata umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni, hasa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.Wanatumia programu hiyo kushirikishana video ya sekunde 15 ambayo mara nyingi hujumuisha kuiga nyimbo fulani, wachekeshaji wakifanya vimbwanga vyao na mifumo isiyo ya kawaida ya kubadilisha picha na vyinginevyo.Video hizo huweza kufikiwa na wafuasi wa programu hiyo na hata wageni. Kimsingi, akaunti zote zinaweza kuonekana na kila mmoja ingawa watumiaji wanaweza kuweka masharti ya video wanazotaka kupakua kwa orodha ya watu kadhaa tu waliowachagua wenyewe.TikTok pia inaruhusu ujumbe wa kibinafsi kutumwa lakini huduma hii ni kwa marafiki pekee.Inasemekana kwamba programu hii ina watumiaji karibu milioni 800 kila mwezi wengi wao wakiwa ni kutoka Marekani na India.India tayari imepiga marufuku programu ya TikTok pamoja na programu zingine za China.Australia, ambayo tayari imeshapiga marufuku kampuni ya Huawei na ile ya utengenezaji bidhaa za mawasiliano ya ZTE, pia inafikiria kupiga marufuku programu ya TikTok.WeChat nayo ilibuniwa 2011. Programu hiyo inawawezesha watumiaji wake kutuma na kupokea ujumbe, kununu a na kulipa bidha kwa kutumia simu na pi akutumia hudama za mtandao za nchi husika na inasifiwa kwa kuwa “programu inayokidhi mahitaji yote” nchini China na ina zaidi ya wateja bilioni moja ambao wanatumia huduma hizo kwa mwezi.Mnamo Machi, ripoti moja ilisema WeChat ilikuwa ikificha taarifa muhimu juu ya kuzuka kwa virusi vya corona tangu Januari mosi.Lakini WeChat inasisitiza usimbaji fiche wa unamaanisha wengine hawawezi “kufikia” kwenye ujumbe wa mteja ikiwa ni pamoja na yaliyomo kama maandishi, sauti na picha hazihifadhiwa kwenye seva zake – na hufutwa mara tu wapokeaji wote waliokusudiwa wamesoma. ,

 

TikTok na WeChat zitapigwa marufuku nchini Marekani kuanzia Jumapili, endapo Rais Donald Trump atakubali kutekeleza mkataba wa dakika za mwisho.

Idara ya biashara ya imesema itawazuia watu nchini Marekani kupakua progamu hizo kupitia mtandao wowote.

Utawala wa Trump unasema kampuni zinazomiliki mitandao hiyo ni tishio kwa usalama wa taifa na kwamba huenda ikwasilisha maelezo ya watumiaji wake kwa China.

Lakini China na kampuni hizo zote mbili zimepinga madai hayo.

WeChat itafungwa rasmi nchini Marekani siku ya Jumapili, lakini watu wataweza kutumia TikTok hadi tarehe 12 Novemba, wakati ambapo pia huenda ikafungwa.

Ikiwa mpango wa ushirikiano kati ya kampuni ya teknolojia ya Marekani, Oracle na mwenyeji wa TikTok ByteDance utakubaliwa na kuidhinishwa na Rais Trump, programu hiyo huenda isipigwe marufuku.

Haijabainika ikiwa bwana Trump ataidhinisha mpango huo, lakini anatarajiwa kutathmini hatua hiyo kabla ya siku ya Jumapili.

 Amri ya marufuku kutoka Idara ya Biashara inafuata amri ya rais iliyotiwa saini mwezi Agosti ambayo iliipatia biashara nchi Marekani siku 45 kuacha kufanya kazi na kampuni hizo mbili za China.

“Kulingana na maelekezo ya rais, tumechukua hatua ya kudhibiti ulaghai wa China dhidi ya kukusanya taarifa binafsi ya watu wa Marekani,” Wiziri ya biashara Wilbur Ross alisema katika taarifa.

Wizara hiyo ilikubali hofu ya kiusalama inayohusishwa na mitandao ya WeChat na TikTok haifanani lakini ilisema kwamba kila moja ilikusanya “maelezo mengi kutoka kwa watumiaji wa huduma yao, ikiwa ni pamoja na, mahali wanapoishi, mfumo wamawasiliano wanaotumia na na historia ya vitu wanavyotafuta mtandaoni”.

Maafisa Marekani na wanasiasa wameonesha wasiwasi wao kuhusu data inayokusanywa na kampuni ya ByteDance kupitia programu ya TikTok kwamba huenda ikakabidhiwa serikali ya China.

Nchini China, TikTok inatoa huduma sawa na hiyo lakini kupitia toleo jinginge la programu ya China inayofahamika kama Douyin.

Pia inasema data ya watumiaji wote wa Marekani inahifadhiwa Marekani huku chelezo cha programu hiyo ikiwa Singapore.Wiki hii, kampuni ya TikTok iliwaambia watumiaji wake na wadhibiti kwamba huenda ikawa na uwazi wa hali ya juu ikiwemo kuruhusu kupitiwa tena kwa mfumo huo.

“Hatuko kisiasa, haturuhusu matangazo ya kisiasa na hatuna ajenda yoyote – lengo letu kuu ni kuendelea kusisimua, kuwa mtandao ambao kila mmoja ataufurahia,” amesema Mkurugenzi mtendaji wa TikTok, Kevin Mayer, wiki hii.

“TikTok imekuwa mlengwa mkuu, lakini sisi sio adui.”

Programu hiyo imepata umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni, hasa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.

Wanatumia programu hiyo kushirikishana video ya sekunde 15 ambayo mara nyingi hujumuisha kuiga nyimbo fulani, wachekeshaji wakifanya vimbwanga vyao na mifumo isiyo ya kawaida ya kubadilisha picha na vyinginevyo.

Video hizo huweza kufikiwa na wafuasi wa programu hiyo na hata wageni. Kimsingi, akaunti zote zinaweza kuonekana na kila mmoja ingawa watumiaji wanaweza kuweka masharti ya video wanazotaka kupakua kwa orodha ya watu kadhaa tu waliowachagua wenyewe.

TikTok pia inaruhusu ujumbe wa kibinafsi kutumwa lakini huduma hii ni kwa marafiki pekee.

Inasemekana kwamba programu hii ina watumiaji karibu milioni 800 kila mwezi wengi wao wakiwa ni kutoka Marekani na India.

India tayari imepiga marufuku programu ya TikTok pamoja na programu zingine za China.

Australia, ambayo tayari imeshapiga marufuku kampuni ya Huawei na ile ya utengenezaji bidhaa za mawasiliano ya ZTE, pia inafikiria kupiga marufuku programu ya TikTok.

WeChat nayo ilibuniwa 2011. Programu hiyo inawawezesha watumiaji wake kutuma na kupokea ujumbe, kununu a na kulipa bidha kwa kutumia simu na pi akutumia hudama za mtandao za nchi husika na inasifiwa kwa kuwa “programu inayokidhi mahitaji yote” nchini China na ina zaidi ya wateja bilioni moja ambao wanatumia huduma hizo kwa mwezi.

Mnamo Machi, ripoti moja ilisema WeChat ilikuwa ikificha taarifa muhimu juu ya kuzuka kwa virusi vya corona tangu Januari mosi.

Lakini WeChat inasisitiza usimbaji fiche wa unamaanisha wengine hawawezi “kufikia” kwenye ujumbe wa mteja ikiwa ni pamoja na yaliyomo kama maandishi, sauti na picha hazihifadhiwa kwenye seva zake – na hufutwa mara tu wapokeaji wote waliokusudiwa wamesoma.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *