Mapokezi Ya Zitto Kigoma Siku Kadhaa Baada Ya Ajali

October 16, 2020

Mgombea ubunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe leo Ijumaa Oktoba 16, 2020 amewasili  mkoani Kigoma ikiwa zimepita siku 10 tangu alipopata ajali ya gari mkoani humo na kuhamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu.

Zitto ambaye ni kiongozi wa chama hicho alipata ajali Oktoba 6, 2020 mkoani humo wakati akielekea katika mkutano wa kampeni jimbo la Kigoma Kusini, akiwa na watu wengine wanne.

Baada ya kufika jijini Dar es Salaam, Zitto alipelekwa katika Hospitali ya Aga Khan na kufanyiwa upasuaji katika bega lake la kushoto.

Leo katika uwanja wa ndege mjini Kigoma wanachama na wafuasi wa chama hicho walifika eneo hilo kuanzia saa 3 asubuhi kwa lengo la kumlaki kiongozi wao huyo ambaye baada ya kushuka kwenye ndege alipokelewa na wanachama hao huku akiwashukuru kwa kumuombea.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *