Mapinduzi Mali: Upinzani wasema kwamba jeshi lina mpango wa kunyakuwa mamlaka kutoka kwa raia

September 13, 2020

Dakika 4 zilizopita

Mapinduzi ya mwezi uliopita yaliungwa mkono na raia

Maelezo ya picha,

Mapinduzi ya mwezi uliopita yaliungwa mkono na raia

Muungano wa Upinzani ambao uliongoza maandamano ya Mali kabla ya kufanyika kwa mapinduzi mwezi uliopita umekataa makubaliano ya serikali ya mpito.

Siku ya Jumamosi , jeshi la taifa hilo lilikubaliana kuweka serikali ya mpito ya miezi 18 hadi pale uchaguzi utakapofanyika.

Makubaliano hayo yanajiri baada ya siku tatu za mazungumzo na upinzani na makundi ya wanaharakati.

Lakini kundi la M5-RFP , ambalo lilihusika katika majadiliano hayo limesema kwamba maafikiano hayo yalikuwa jaribio la jeshi ‘kunyakua mamlaka’.

Pia lilisema kwamba makubaliano hayo hayakutilia maanani kile ilichosema kwamba atakeyeongoza serikali hiyo ya mpito anapaswa kutoka kwa upande wa raia na kwamba hayakuafikia maoni ya raia wa Mali.

Shirika la mataifa ya magharibi mwa Africa Ecowas , pia lilikuwa limetoa wito wa rais wa mpito kuwa raia, lakini uongozi wa jeshi unasema kwamba raia ama mwanajeshi anaweza kuongoza.

Masharti ya serikali hiyo ya mpito yaliotolewa na viongozi wa kijeshi pia yanasema kwamba bodi ya mpito ilio na wanachama wa M5-RFP itaundwa.

Mali inakumbwa na msukosuko wa wapiganaji wa Kiislamu na ghasia za kikabila pamoja na uchumi unaozorota.

Muhariri wa BBC wa Afrika Mary Harper anasema kwamba hali ya wasiwasi kati ya jeshi na kundi lililoongoza maandamano dhidi ya rais aliyepinduliwa Ibrahim Boubavcar Keita inatishia amani zaidi

Je ni nini kilichomtokea rais wa zamani?

Rais aliyeondolewa madarakani alielekea UAE kwa matibabu tarehe 5 mwezi Septemba baada ya kuugua kiharusi , kulingana na maafisa wa jeshi .

Afisa wake mkuu wa serikali aliokuwa akiongoza anasema kwaba huenda ikamchukua hadi siku 15.

Baada ya mapinduzi hayo , viongozi wa mataifa ya magharibi walisema kwamba wanataka kurudi haraka kwa uongozi wa kiraia.

Viongozi wa jeshi nchini Mali awali walikuwa wamesema kwamba serikali ya mpito itahudumu kwa kipindi cha miaka miwili.

Rais Keita alipinduliwa tarehe 18 Agosti kufuatia maandamano makubwa dhidi ya ufisadi , usimamizi mbaya wa kiuchumi na mgogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi wa ubunge.

Mapinduzi hayo yalisababisha shutuma za kimataifa , lakini yaliungwa mkono na raia wa Mali. Bwana Keita alikamatwa na jeshi lakini baadaye akaachiliwa.

Rais aliyeondolewa madarakani Boubacar Keita alitoroka taifa hilo wiki iliopita

Maelezo ya picha,

Rais aliyeondolewa madarakani Boubacar Keita alitoroka taifa hilo wiki iliopita

Haya yalikuwa mapinduzi ya nne katika taifa hilo la Afrika magharibi tangu lilipojipatia uhuru kutoka kwa Ufaransa 1960.

Mapinduzi ya awali 2012 yaliwapatia nguvu wapiganaji wa Kiislamu walioliteka eneo la kaskazini mwa Mali.

Wanajeshi wa Ufaransa walilikomboa eneo hilo lakini mashambulizi yanaendelea.

Viongozi wa mapinduzi hayo awali walikuwa wameahidi kuheshimu makubaliano ya kimataifa kuhusu kupigana na Wanajihad.

Maelfu ya vikosi vya Ufaransa, Afrika na Umoja wa mataifa vimepiga kambi nchini humo kukabiliana na wapiganaji hao.

Source link

,Dakika 4 zilizopita Chanzo cha picha, EPA Maelezo ya picha, Mapinduzi ya mwezi uliopita yaliungwa mkono na raia Muungano wa…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *