Mapigano yanaendelea Afghanistan pamoja na kuanza mazungumzo ya amani, on September 13, 2020 at 5:00 pm

September 13, 2020

Vikosi vya Taliban na serikali vimekabiliana kwa muda wa masaa kadhaa katika maeneo tofauti ya Afghanistan, ikiwa ni baada ya kuanza kwa mazungumzo ya amani ambayo yalikuwa yanasubiriwa kwa muda mrefu.Mazungunzo hayo ya mani yameanza jana mjini Doha, Qatar. Hali hiyo inaongeza changamoto ya kuvimaliza vita vilivyodumu kwa miaka 19. Mashambulizi ya Taliban ya usiku wa Jumamosi yamethibitshwa na maafisa wa majimbo ya Kapsia na Kunduz.Katika taarifa yake Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid inasema wanamgambo wa kundi hilo wameushambulia msafara wa wanajeshi wa Afghanistan wakiwa katika barabara kubwa ya kuelekea Kunduz, na kuongoza kwamba vikosi vya serikali vilifanya mashambulizi ya anga na kutumia mizinga katika majimbo ya Baghlan na Jowzjan.,

Vikosi vya Taliban na serikali vimekabiliana kwa muda wa masaa kadhaa katika maeneo tofauti ya Afghanistan, ikiwa ni baada ya kuanza kwa mazungumzo ya amani ambayo yalikuwa yanasubiriwa kwa muda mrefu.

Mazungunzo hayo ya mani yameanza jana mjini Doha, Qatar. Hali hiyo inaongeza changamoto ya kuvimaliza vita vilivyodumu kwa miaka 19. Mashambulizi ya Taliban ya usiku wa Jumamosi yamethibitshwa na maafisa wa majimbo ya Kapsia na Kunduz.

Katika taarifa yake Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid inasema wanamgambo wa kundi hilo wameushambulia msafara wa wanajeshi wa Afghanistan wakiwa katika barabara kubwa ya kuelekea Kunduz, na kuongoza kwamba vikosi vya serikali vilifanya mashambulizi ya anga na kutumia mizinga katika majimbo ya Baghlan na Jowzjan.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *