Mapigano makali yaripotiwa Nagorno-Karabakh,

October 3, 2020

 

Vikosi vya Azerbaijan vimeanzisha upya mashambulizi makali kwenye eneo lenye mzozo la Nagorno-Karabakh na vimesonga mbele kutoka pande mbili za kusini na kaskazini ya jimbo hilo. 

Hayo ni kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Armenia iliyozungumzia kuwepo kwa mapigano makali kwenye eneo hilo linalodhibitiwa na wakaazi wenye asili ya Armenia wanaongoza kampeni ya kujitenga kutoka Azerbaijan.

 Hata hivyo, imekuwa vigumu kuthibitisha taarifa hizo za Armenia ikiwa ni pamoja na madai kuwa imezidungua ndege tatu za kivita za Azerbaijan. Madola yenye nguvu duniani yamekuwa yakitoa wito wa kusitishwa mapigano baina ya mataifa hayo hasimu yaliyozuka Juamapili iliyopita kuwania jimbo la Nagorno-Karabakh linalotambulika kuwa sehemu ya Azerbaijan. 

Vyanzo kutoka Armenia vinasema hadi kufikia sasa mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 200, lakini upande wa Azerbaijan unasema ni watu 19 pekee wamekufa na wengine 60 wamejeruhiwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *