Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan yapamba moto

October 5, 2020

Vikosi vya Armenia na Azerbaijan vimeshambuliana kwa maroketi na makombora wakati ambapo mapigano yanazidi kwenye eneo la Nagorno-Karabach. 

Armenia imesema kuwa mji mkuu wa Nagorno-Karabach, Stepanakert ambao umekuwa ukishambuliwa kwa makombora tangu Ijumaa, umeshambuliwa tena jana. 

Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan imesema vikosi vya Armenia vimeushambulia mji wa Ganja, huku picha zikionyesha kuharibiwa vibaya kwa majengo.

 Jana usiku, Hikmet Hajiyev, mshauri wa Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba vikosi vya Armenia vimeanzisha mashambulizi ya makombora dhidi ya raia wa Azerbaijan na miundombinu ya raia, kwenye mji wa Mingechavir, umbali wa kilomita 80 kutoka kwenye mji mkuu, Baku. 

Nchi hizo mbili zimepinga wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano na badala yake zimezidisha mapigano katika siku za hivi karibuni, huku kila upande ukitangaza kushinda

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *