Maofisa watano wa polisi wafukuzwa kazi kwa tuhuma za kuharibu ushahidi wa tukio la ubakaji India,

October 5, 2020

Maofisa 5 akiwemo Kamanda wa Wilaya wameachishwa kazi wakituhumiwa kuharibu ushahidi wa tukio la binti wa miaka 19 kubakwa na kuuawa na kundi la wahuni jambo lililosababisha maandamano ya watu

Polisi hao wanatuhumiwa kuchelewesha usajili wa kesi pamoja na malalamiko ya ndugu wa marehemu na pia walifanya maamuzi ya kuuchoma mwili wa marehemu bila ridhaa ya familia yake

Aidha, Polisi wamekosolewa na jamii wakidaiwa kuvizuia Vyombo vya Habari na Vyama vya Siasa vya Upinzani kuongea na familia ya marehemu

Marehemu alifanyiwa ukatili huo na wanaume 4 katika eneo lililo karibu na kijiji alichokuwa anaishi Kaskazini mwa #India

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *