Makubaliano ya mafuta: Tanzania kujipatia faida ya asilimia 60 nayo Uganda ikipata asilimia 40

September 13, 2020

Dakika 16 zilizopita

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika picha ya awali

Maelezo ya picha,

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika picha ya awali

Viongozi wa Tanzania na Uganda hatimaye wamekubaliana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka mji wa Hoima nchini Uganda hadi changalieni mjini TangaTanzania.

Katika makubaliano hayo yaliotiwa saini na mawaziri wa nishati kutoka pande hizo mbili na marais wa mataifa hayo mawili John Pombe Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda katika eneo la Chato , asilimia 60 ya faida ya mafuta hayo itaenda kwa Tanzania huku asilimia 40 ikienda kwa Uganda.

Akizungumza katika hafla hiyo , rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema kwamba cha muhimu ilikuwa kuanza mradi huo aliodai kucheleweshwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

”Niliamua kwamba kucheleweshwa kwa mradi huu kwasababu ya zile dola milioni 800 sio jambo la akili kwasababu tunazugumnzia kuzalisha mapipa bilioni 6.5 ikiwa ni asilimia 40 pekee ya mafuta yaliogunduliwa katika eneo la Albert, lakini huenda tukapata mafuta hata zaidi katika eneo hilo”, alisema.

Rais Museveni akihutubia uma baada ya kutia saini mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania

Maelezo ya picha,

Rais Museveni akihutubia uma baada ya kutia saini mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania

Kiongozi huyo amesema kwamba uwekezaji wa bomba hilo la mafuta utagharimu dola bilioni 4 za Marekani.

”Niliamua kwamba wacha tuwache kuchelewesha tuanze mradi. Tuliongea kwa simu mimi na mdogo wangu, nikamwambia achukue hata asilimia 70 au 80 lakini mdogow angu akaona aibu akasema asilimia 60 inakwenda Tanzania, 40 inaenda Uganda.

Awali akizungumza , rais Magufuli amesema kwamba mradi huo utaimarisha uchumi wa mataifa haya mawili na eneo lote la Afrika mashariki na kati.

Alisema kwamba mataifa yaliopo katika ushoroba wa kaskazini yatafaidika pakubwa na bomba hilo.

Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania
Maelezo ya picha,

Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania

Rais Magufuli akimpongeza rais Museveni baada ya kutia saini uanzishaji wa ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Uganda hadi Tanzania

Maelezo ya picha,

Rais Magufuli akimpongeza rais Museveni baada ya kutia saini uanzishaji wa ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Uganda hadi Tanzania

Amesema kwamba takriban Watanzania kati ya 10,000 na hadi 15,000 watafaidika na ajira za kazi mradi huo utakapo kamilika.

”Litakuwa bomba refu zaidi duniani lenye teknolojia ya sasa ya kusafirisha mafuta yakiwa katika joto”, alisema magufuli

Amesema kwamba bomba hilo litakuwa refu zaidi duniani linalotumia teknolojia ya kupasha moto mafuta likiwa na urefu wa kilomita 1445.

Kilomita 1115 za bomba hilo zitakuwa upande wa Tanzania 330 zitakuwa upande wa Tanzania.

Rais Magufuli amesema kwamba mradi huo utapitia mikoa minane ikiwemo wilaya 24. Mikoa hiyo ni Kagera, Geita , Shinyanga , Tabora, Singida, Dodoma, Manyara, na Tanga.

Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga
Maelezo ya picha,

Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga

Magufuli amesema kwamba watu 90,000 watakaoathiriwa mashamba yao watalipwa fidia ya bilioni 21 fedha za Tanzania.

Ameongezea kwamba Ujenzi wa vituo 14 vya bomba hilo vitawafidia watakaoathiriwa 9.9 za Tanzania.

Source link

,Dakika 16 zilizopita Chanzo cha picha, Ikulu ya rais Tanzania Maelezo ya picha, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *