Makamu wa Rais wa Afghanistan ajeruhiwa katika mripuko wa Kabul

September 9, 2020

Makamu wa Rais wa Afghanistan Amrullah Saleh amenusurika kwenye jaribio la mauaji dhidi yake baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bomu, ambalo limewauwa karibu watu 10 na kuwajeruhi wengine kadhaa, karibu na mji mkuu, Kabul. Mara tu baada ya mripuko huo, Saleh, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Taliban, alisema alikuwa njiani kwenda ofisini kwake wakati msafara wake ulishambuliwa. Amesema yupo salama licha ya kupata majehara madogo tu ya kuungua usoni na mikononi. Mwanawe wa kiume ambaye alikuwa naye kwenye gari, pia yuko salama. Tariq Arian ni msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan. Shambulizi hilo lililaaniwa mara moja kama jaribio la kuuhujumu mchakato wa kutafuta amani nchini Afghanistan, lililofanywa wakati serikali ikijiandaa kuwatuma wajumbe wake nchini Qatar kwa mazungumzo yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu na Taliban.,

Makamu wa Rais wa Afghanistan Amrullah Saleh amenusurika kwenye jaribio la mauaji dhidi yake baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bomu, ambalo limewauwa karibu watu 10 na kuwajeruhi wengine kadhaa, karibu na mji mkuu, Kabul.

 Mara tu baada ya mripuko huo, Saleh, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Taliban, alisema alikuwa njiani kwenda ofisini kwake wakati msafara wake ulishambuliwa. 

Amesema yupo salama licha ya kupata majehara madogo tu ya kuungua usoni na mikononi. Mwanawe wa kiume ambaye alikuwa naye kwenye gari, pia yuko salama. Tariq Arian ni msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan.

 Shambulizi hilo lililaaniwa mara moja kama jaribio la kuuhujumu mchakato wa kutafuta amani nchini Afghanistan, lililofanywa wakati serikali ikijiandaa kuwatuma wajumbe wake nchini Qatar kwa mazungumzo yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu na Taliban.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *