Makaburi ya Misri: Majeneza yaliozikwa miaka 2,500 yafukuliwa Saqqara

September 21, 2020

Dakika 1 iliyopita

Majeneza hayo yalipatikana katika kisima kipya kilichogunduliwa katika eneo moja takatifu lililopo huko Saqqara

Maelezo ya picha,

Majeneza hayo yalipatikana katika kisima kipya kilichogunduliwa katika eneo moja takatifu lililopo huko Saqqara

Jumla ya majeneza 27 yaliozikwa zaidi ya miaka 2500 yamefukuliwa na wanakiolojia katika makaburi ya zamani nchini Misri.

Majeneza hayo yalipatikana katika kisima kipya kilichogunduliwa katika eneo moja takatifu lililopo huko Saqqara , kusini mwa mji mkuu wa Cairo.

Majeneza 13 yaligunduliwa mapema mwezi huu , lakini mengine 14 zaidi yamepatikana , maafia wanaesma.

Ugunduzi huo unasemekana na wataalamu kuwa mkubwa zaidi kuwahi kufanyika.

Picha zilizotolewa zinaonesha majeneza yaliopakwa rangi za kuvutia na kuhifadhiwa na vitu vingine vidogo.

Saqqara lilikua maziko ya watu wengi kwa zaidi ya miaka 3000 na limeorodhedhwa miongoni mwa turathi duniani.

“Utafiti wa awali unaonesha kwamba majeneza hayo yalikuwa yamefungwa kabisa na kwamba hayajawahi kufunguliwa tangu yalipozikwa , alisema waziri wa mambo ya kale nchini Misri katika taarifa siku ya Jumamosi.

‘Siri zaidi’

Taarifa hiyo inaongeza kwamba waziri wa mambo ya kale nchini Misri Khaled al-Anani awali alichelewesha kutangaza ugunduzi huo hadi pale alipotembelea eneo hilo mwenyewe , ambapo aliwashukuru wafanyakazi kwa kufanya kazi katika hali ngumu chini ya kisima hicho chenye urefu wa mita 11..

Wafanyakazi walilazimika kuingi katika kisima hicho kirefu

Maelezo ya picha,

Wafanyakazi walilazimika kuingi katika kisima hicho kirefu

1px transparent line

Uchimbuaji unaendelea katika eneo hilo huku wataalamu wakijaribu kujua maelezo zaidi kuhusu chanzo cha majeneza hayo.

Wataalamu wanasema kwamba majeneza hayo yalikuwa hayajafunguliwa tangu yalipozikwa

Maelezo ya picha,

Wataalamu wanasema kwamba majeneza hayo yalikuwa hayajafunguliwa tangu yalipozikwa

Waziri huyo alisema kwamba alitumai kwamba ugunduzi huo utazidi kufumbua ‘siri zaidi’ katika mkutano na wanahabari katika sku zijazo.

Baadhi ya majeneza yalipambwa na rangi tofauti za kuvutia

Maelezo ya picha,

Baadhi ya majeneza yalipambwa na rangi tofauti za kuvutia

1px transparent line

Vitu vingine vya kale vilivyogunduliwa karibu na majeneza hayo ya mbao pia vilionekana vimeundwa kwa mandhari mazuri na kupakwa rangi za kuvutia.

line
Mojawapo ya vitu hivyo vya kale vilivyopatikana karibu na majeneza hayo ya Saqqara

Maelezo ya picha,

Mojawapo ya vitu hivyo vya kale vilivyopatikana karibu na majeneza hayo ya Saqqara

1px transparent line

Mnamo mwezi Novemba 2018 , kiwango kikubwa cha wanyama waliokaushwa na kuhifadhiwa karibu na Saqqara walioneshwa kwa umma kwa mara ya kwaza. Ugunduzi huo ulihusisha paka , mamba, nyoka aina ya kobra na ndege.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Watch footage of the mummified big cats on display at the exhibition

Eneo la Saqqara, lililopo kilomita 30 kusini ma mji wa Cairo , ni eneo lenye makaburi ya zamani ambalo pia lilikuwa likihudumu kama eneo la maziko la mji mkuu wa zamani wa Misri Memphis, kwa zaidi ya miongo miwili.

Katika miaka ya hivi karibuni , Misri imezidisha ukuzaji wake wa ugunduzi wa vitu vya kale kwa lengo la kufufua utalii wake

Source link

,Dakika 1 iliyopita Chanzo cha picha, EPA Maelezo ya picha, Majeneza hayo yalipatikana katika kisima kipya kilichogunduliwa katika eneo moja…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *