Majaji wa rufaa ICC waunga mkono kushikiliwa kwa mshukiwa wa Darfur,

October 8, 2020

 

Majaji wa rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wameunga mkono kuwekwa kizuwizini kwa mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa wanamgambo wa Sudan anayetuhumiwa kwa makosa zaidi ya 50 ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita katika mkoa wa Darfur. 

Ali Mohammed Ali Abdul Rahman Ali, maarufu kama Ali Khushayb, amekuwa katika kizuwizi cha mahakama hiyo ya kimataifa tangu alipohamishiwa katika makao makuu yake mjini The Hague mwezi Juni, zaidi ya miaka 13 bada ya kutolewa kwa waranti wa kwanza wa kukamatwa kwake. 

Kufuatia kuhamishiwa kwake katika mahakama hiyo ya ICC, Khushayb aliomba kuachiwa kwa muda kutokana kizuwizi cha mahakama wakati kesi yake ikiendelea. 

Majaji walikataa ombi lake, na leo hukumu ya kamati ya rufaa imethibitisha uamuzi huo. Mahakama itaamuwa Desemba 7, iwapo upande wa mashtaka una ushahidi wa kutosha kuwezesha uendeshaji wa kesi kamili.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *