Mahakama yamuukumu miaka miwili jela mwanamke aliejikata mkono ili alipwe na bima, on September 14, 2020 at 8:00 am

September 14, 2020

Mahakama Jijini Ljubljana nchini Slovenia imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela, mwanamke aliyejikata mkono wake wa kushoto akitarajia kulipwa zaidi ya £925,000 kama fidia ya matibabu kupitia mashirika ya bima.Julija Adlesic mwenye umri wa miaka 22, alibainika kuwa alipanga na mpenzi wake kuukata mkono wake kwa makusudi wakiwa nyumbani kwao katika Jiji hilo, mapema mwaka 2019.Baada ya uchunguzi wa kina, Adlesic alikutwa na hatia ya kujaribu kufanya udanganyifu ili kujipatia fedha kwenye mashirika ya bima, alikata bima za afya kwenye mashirika kadhaa mwaka mmoja kabla.Kwa mujibu wa sheria za bima, endapo tukio hilo la kukata mkono lingeonekana ni halisi, angelipwa nusu ya kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matibu punde tu baada ya kuripoti tukio, na kiasi kingine kingeendelea kulipwa.,

Mahakama Jijini Ljubljana nchini Slovenia imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela, mwanamke aliyejikata mkono wake wa kushoto akitarajia kulipwa zaidi ya £925,000 kama fidia ya matibabu kupitia mashirika ya bima.

Julija Adlesic mwenye umri wa miaka 22, alibainika kuwa alipanga na mpenzi wake kuukata mkono wake kwa makusudi wakiwa nyumbani kwao katika Jiji hilo, mapema mwaka 2019.

Baada ya uchunguzi wa kina, Adlesic alikutwa na hatia ya kujaribu kufanya udanganyifu ili kujipatia fedha kwenye mashirika ya bima, alikata bima za afya kwenye mashirika kadhaa mwaka mmoja kabla.

Kwa mujibu wa sheria za bima, endapo tukio hilo la kukata mkono lingeonekana ni halisi, angelipwa nusu ya kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matibu punde tu baada ya kuripoti tukio, na kiasi kingine kingeendelea kulipwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *