Mahakama yamuidhinisha Condé kugombea muhula wa tatu Guinea, on September 10, 2020 at 1:00 pm

September 10, 2020

Mahakama ya kikatiba nchini Guinea imemuidhinisha rais Alpha Condé mwenye umri wa miaka 82 kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu utakaoandaliwa mwezi ujao.Mahakama hiyo pia imewaidhinisha wagombea 11, miongoni mwao mgombea mkuu wa upinzani Cellou Dalein Diallo.Miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya bwana Condé baada ya kiongozi huyo kushinikiza mageuzi ya kikatiba kupitia kura ya maoni ya mwezi Maachi iliyomwezesha kugombea muhula wa tatu.Karibu wa 30 wameripotiwa kuuawa katika maandamano hayo.Bwana Condé alichaguliwa mara ya kwanza 2010 na kisha kuchaguliwa tena kwa mara ya pili 2015.Siku ya Jumanne, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alitoa wito kwa viongozi wa Afrika Magharibi kuzingatia ukomo wa mihula yao madarakani kwa mujibu wa katiba -ambayo alitaja kuwa chanzo cha mizozo ya kisiasa katika eneo hilo.,

Mahakama ya kikatiba nchini Guinea imemuidhinisha rais Alpha Condé mwenye umri wa miaka 82 kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu utakaoandaliwa mwezi ujao.

Mahakama hiyo pia imewaidhinisha wagombea 11, miongoni mwao mgombea mkuu wa upinzani Cellou Dalein Diallo.

Miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya bwana Condé baada ya kiongozi huyo kushinikiza mageuzi ya kikatiba kupitia kura ya maoni ya mwezi Maachi iliyomwezesha kugombea muhula wa tatu.

Karibu wa 30 wameripotiwa kuuawa katika maandamano hayo.

Bwana Condé alichaguliwa mara ya kwanza 2010 na kisha kuchaguliwa tena kwa mara ya pili 2015.

Siku ya Jumanne, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alitoa wito kwa viongozi wa Afrika Magharibi kuzingatia ukomo wa mihula yao madarakani kwa mujibu wa katiba -ambayo alitaja kuwa chanzo cha mizozo ya kisiasa katika eneo hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *