Mahakama ya Saudi Arabia yawapungunzia adhabu waliomuua Jamal Khashoggi

September 8, 2020

Dakika 5 zilizopita

Jamal Khashoggi
Maelezo ya picha,

Waendesha mashitaka wamesema kuwa walipewa hukumu ya miaka 20 jela baada ya baada ya familia ya Khashogi ambaye alikuwa ni mwaandishi wa habari kuamua kuwasamehe

Mahakama nchini Saudi Arabia imeondoa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watu watano waliopatikana na hatia ya mauaji ya Jamal Khashoggi, mwaka 2018, vimesema vyombo vya habari.

Waendesha mashitaka wamesema kuwa walipewa hukumu ya miaka 20 jela baada ya familia ya Khashoggi ambaye alikuwa ni mwaandishi wa habari kuamua kuwasamehe.

Hatahivyo, mchumba wake amesema uamuzi uliofanywa ni “ni kejeli ya haki kabisa”

Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji maarufu wa serikali ya Saudia aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Ufalme wa Saudia katika mji mkuu wa Uturuki Instanbul na maafisa wa ujasusi wa Saudi Arabia.

Serikali ya Saudia ilisema kuwa mwandishi huyo wa habari aliuawa katika “operesheni ambayo haikukusudiwa ” na mwaka uliofuatia Saudi Arabia iliwashitaki watu 11 mahakamani kuhusiana na kifo hicho.

Kesi hiyo ilipuuziliwa mbali mara tatu na Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Agnes Callamard aliyeitaja kama “isiyofuata sheria ” ambaye alisema kuwa Khashoggi alikuwa “muathiriwa wa mauaji ya makusudi, yaliyopangwa ” ambayo taifa la Saudi Arabia linawajibika nayo.

Bi Callamard alisema kuna ushahidi wa kuaminika kwamba maafisa wa ngazi ya juu, akiwemo Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, wanahusika binafsi.

Mwanamfalme alikana kuhusika, ingawa washirika wake wawili wa zamani wanashitakiwa bila kuwepo mahakamani nchini Uturuki kwa kosa la kupanga mauaji ya Khashoggi. Wasaudia wengine kumi na wanane wanashutumiwa kwa kutekeleza mauaji hayo.

Jamal Khashoggi alikufa vipi?

Khashoggi mwandishi wa habari ambaye alikuwa na umri wa miaka 59-ambaye alikwenda uhamishoni nchini Marekani mwaka 2017, alionekana mara ya mwisho akiingia katika ubalozi wa Saudi Arabia tarehe 2 Octoba 2018 kuchukua makaratasi aliyokuwa akiyahitaji ili aweze kumuoa mchumba wake Mturuki , Hatice Cengiz.

Baada ya kusikiliza kile kinachodaiwa kuwa ni sauti ya mazungumzo ndani ya ubalozi iliyotengenezwa na idara ya ujasusi ya Uturuki, Bi Callamard alisema kwamba Khashoggi “aliuawa kikatili na watu wengi ” siku ile.

Waendesha mashitaka wa umma nchini Saudia Arabia walisema kuwa mauaji hayo yalipangwa kabla ya kutekelezwa.

Walisema kuwa mauaji hayo yaliamrishwa na mkuu wa “maafisa wa upatanishi ” aliyetumwa Istanbul kumrudisha Khashoggi katika Ufalme wa Saudia “kwa njia ya kumshawishi ” au , kama hilo litashindikana “kwa nguvu “.

Mwandishi huyo wa habari alilazimishwa kunyamaza baada ya kuhangaika na kudungwa kiwango kikubwa cha dawa, ambayo matokeo yake ilipita kiwango cha dozi ambayo ilisababisha kifo chake, kwa mujibu wa waendesha mashitaka. Hatimae mwili wake ulikatwa katwa na kukabidhiwa kwa “washirika” wa mauaji hayo wa Uturuki nje ya ubalozi . Mabaki ya mwili wake hayakuwahi kupoatikana .

Waendesha mashitaka wa Uturuki walisema kwamba Khashoggi alibanwa pumzi yake mara alipoingia katika ubalozi, na kwamba mwili wake uliharibiwa.

Mwezi Disemba 2019 mahakama ya uhalifu ya Riyadh iliwahukumu watu watano kifo kwa ” ”kutekeleza na kushiriki moja kwa moja mauaji ya muathiriwa” . Wengine watatu walipewa athabu ya kifungo cha jela cha jumla ya miaka 24 kwa “kuficha uhalifu huu na ukiukaji wa sheria “.

Watu watatu hawakupatikana na hatia, ikiwa ni pamoja na Naibu mkuu wa zamani wa ujasusi wa Saudi Arabia , Ahmad Asiri.

Saud al-Qahtani, mshauri wa zamani wa ngazi ya juu wa Mwanamfalme Mohammed, alichunguzwa na waendesha mashitaka wa umma wa Saudia lakini hakuhushitakiwa.

Ni kwanini hukumu ilibadilishwa?

Mwezi Mei mwaka huu, mtoto wa kiume wa Khashoggi Salah alitangaza kuwa yeye na kaka zake ” wanawasamehe wale waliomuua baba yetu, tukitaka kupata zawadi kutoka kwa mwenyezi Mungu”, wakiafiki madai kuwa mauaji hayo hayakupangwa.

Mwanawe Khashoggi Salah alikutana na mfalme wa Saudia na mwanamfalme wiki chache tu baada ya mauaji ya Jama Khashogghi

Maelezo ya picha,

Mwanawe Khashoggi Salah alikutana na mfalme wa Saudia na mwanamfalme wiki chache tu baada ya mauaji ya Jama Khashogghi

Hili lilitoa fursa chini ya sheria za Saudi Arabia kubadilisha hukumu kwa watu watano wanaokabiliwa na hukumu ya kifo.

Jumatatu, Waendesha mashitaka wa umma walitangaza kuwa Mahakama ya uhalifu ya Riyadh imewahukumu watu watano kati ya wale waliopatikana na hatia mwezi Januari kifungo cha miaka 20 jela, na kwamba wengine watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka kati ya saba na 10 jela.

Walisema maamuzi hayo ya mahakama ni ya mwisho na kesi hiyo ya uhalifu imefungwa.

Bi Cengiz alisema katika taarifa yake : “Hukumu iliyotolewa leo nchini Saudi Arabia mwa mara nyingine ni kejeli ya haki”

“Mamlaka nchini Saudia zinafunga kesi bila dunia kujua ukweli wa ni nani aliyehusika na mauaji ya Jamal. Ni nani aliyeyapanga, aliye yaamrisha, mwili wake uko wapi? Haya ni maswali ya kimsingi na muhimu zaidi ambayo bado hayajajibiwa kabisa .”

Mchumba wa Jamal Khashoggi Hatice Cengiz

Maelezo ya picha,

Mchumba wa Jamal Khashoggi Hatice Cengiz

Bi Callamard aliafiki kwamba hukumu ya kifo imeondolewa, lakini amesema kuwa hukumu haingeruhusu “kufuata kile kilichotokea “.

“Waendesha mashitaka wa Saudia walifanya kitendo kingine zaidi katika utekelezaji huu wa sheria. Lakini hukumu hizi hazina sheria wala uhalali wa kimaadili .

Zimekuja katika mwisho wa mchakato ambao haukua wa usawa, hakuna haki, wala uwazi ,” alisema kwenye ujumbe wake wa Tweeter.

Bi Callamard alisema Mwanamfalme Mohammed “ameendelea kulindwa dhidi ya aina yoyote ya uchunguzi muhimu ” na akaitaka idara ya ujasusi ya Marekani kutoa ripoti yao ya tathmini iliyoagizwa juu ya mauaji ya Khashoggi.

Source link

,Dakika 5 zilizopita Maelezo ya picha, Waendesha mashitaka wamesema kuwa walipewa hukumu ya miaka 20 jela baada ya baada ya…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *