Magufuli “Msiniletee magunzi ya Mahindi”, on September 6, 2020 at 6:00 pm

September 6, 2020

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli, amewataka wananchi kuhakikisha endapo wakichagua Rais kutoka chama hicho, basi wahakikishe hata Wabunge na madiwani na wenyewe wanatoka chama hicho, na kudai kuwa hataki kupelekewa magunzi kwa kuwa hakutakuwa na mahusiano ya moja kwa moja.Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 6, 2020, mkoani Mwanza wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Magu, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali ya Tanzania”Kama mnanipenda mimi na mnampenda Kiswaga lazima mtaniletea Madiwani wa CCM, hauwezi ukawa na waya wa umeme halafu katikati ukaweka kamba ya katani, unadhani umeme utawaka?, au unatochi juu ukaweka betri halafu ukaweka gunzi, tochi itawaka? msiniletee magunzi ya mahindi mimi”, amesisitiza Magufuli.Aidha Magufuli ameongeza kuwa “Nimesimama hapa Magu kumuombea kura Kiswaga, wengine wanasema hana degree, kwani nyie mnachagua degree au mtumishi, kwani degree zitakuwa zinawasaidia kuondoa shida, mimi Kiswaga namfahamu mpaka kwao, kwani Musa alikuwa na Degree?”.,

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli, amewataka wananchi kuhakikisha endapo wakichagua Rais kutoka chama hicho, basi wahakikishe hata Wabunge na madiwani na wenyewe wanatoka chama hicho, na kudai kuwa hataki kupelekewa magunzi kwa kuwa hakutakuwa na mahusiano ya moja kwa moja.

Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 6, 2020, mkoani Mwanza wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Magu, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali ya Tanzania

“Kama mnanipenda mimi na mnampenda Kiswaga lazima mtaniletea Madiwani wa CCM, hauwezi ukawa na waya wa umeme halafu katikati ukaweka kamba ya katani, unadhani umeme utawaka?, au unatochi juu ukaweka betri halafu ukaweka gunzi, tochi itawaka? msiniletee magunzi ya mahindi mimi”, amesisitiza Magufuli.

Aidha Magufuli ameongeza kuwa “Nimesimama hapa Magu kumuombea kura Kiswaga, wengine wanasema hana degree, kwani nyie mnachagua degree au mtumishi, kwani degree zitakuwa zinawasaidia kuondoa shida, mimi Kiswaga namfahamu mpaka kwao, kwani Musa alikuwa na Degree?”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *