Magufuli “Hata Sikutegemea Kuwa Rais wa Tanzania…Sikuhonga Wala Kutumwa”

October 12, 2020

 

“Mimi hata sikutegemea kuwa Rais, nimefanya kazi katika kipindi changu cha miaka 5 kwa sababu urais niliupata bila kutumwa na mtu wala kuhonga, mimi nilijua Mungu alinipa kama sadaka ya kuwafanyia kazi Watanzania” Rais MAGUFULI Akiwa DSM

 

“Tulipoingia tu mwanzoni kulikuwa na maeneo hayana amani, Kibiti watu wameuawa mpaka maaskari zaidi ya 17 walipigwa risasi, hiyo ndiyo ilikuwa ‘challenge’ yangu ya kwanza, watu walikuwa wanaibiwa mchana nikasema lazima nikomeshe”

 

“Barabara zilikuwa ni shida watu walikuwa wanakwama masaa 4, wapo wanaume waliokuwa wanaitumia hiyo kuwadanganya wake zao, wako wanawake pia waliowadanganya waume zao, pia wako watoto wetu waliopata mimba kwa sababu ya foleni”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *