Magufuli: Dkt. Bashiru Alikuwa Muuza Ndizi Kemondo

September 15, 2020

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli,  amesema kuwa mkoa wa Kagera una viongozi wengi ambao wamekuwa msaada kwa chama hicho pamoja na serikali kwa jumla, hivyo ataendelea kuwapa nafasi ya kulitumikia taifa hilo hata kama wakisema wamestaafu siasa.Magufuli amesema hayo leo Jumanne, Septemba 15, 2020, wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kasharunga akiwa katika kampeni zake za kuwania urais ambapo ameingia mkoani Kagera.“Miaka mitano iliyopita tulikuja kuomba kura hapa, Prof. Tibaijuka namfahamu tangu zamani, mumewe alikuwa Balozi Sweden mimi nikiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge mwaka 1995 nilikwenda huko, ndiyo maana alipogombea nilikuja nikawaomba mpeni Prof. Tibaijuka.“Aliyekuwa Mbunge wa hapa (Masilingi) kabla ya Mama Tibaijuka alikuwa rafiki yangu, tumehangaika naye kwenye mabarabara, ndiyo maana alipomaliza muda wake nikamteua kuwa Balozi Marekani mpaka leo, ndiyo faida ya kuteua unayemfahamu.“Palikuwa na diwani hapa alikuwa rafiki yangu, alikuwa akitusumbua sana, alikuwa wa chama kingine, nikasimama hapa akasema amehamia CCM leo ni Katibu wa CCM wa Wilaya, hata Mama Tibaijuka anasema amestaafu siasa lakini kwangu nasema hajastaafu.“Huyu Dkt. Bashiru hakuna mtu alitegemea atakuwa Katibu Mkuu wa CCM Tanzania nzima, alikuwa muuza ndizi pale Kemondo, baadaye akaenda Chuo Kikuu Dar es Salaam na leo ndiyo Katibu Mkuu wa CCM Taifa.“Mchakato wa kura za maoni ulipomalizika wa kwanza mpaka wa nne wote wametoka Nshamba, tulichambua tukasema:  Je, tumrudishe aliyekuwa wa kwanza, Katibu wa Prof. Tibaijuka anayelaumiwa hata nyumbani hajajenga nyumba? Tukamteua aliyejenga mpaka shule ya sekondari.“Serikali hii ina vyeo vingi, Prof. Tibaijuka ameniambia mdogo wangu mimi nimestaafu, sasa nasema hujastaafu, hatuwezi kumuacha Profesa hivihivi kwa sababu kuna maeneo mengi ya kufanya kazi,”  amesema Dkt. Magufuli.,

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli,  amesema kuwa mkoa wa Kagera una viongozi wengi ambao wamekuwa msaada kwa chama hicho pamoja na serikali kwa jumla, hivyo ataendelea kuwapa nafasi ya kulitumikia taifa hilo hata kama wakisema wamestaafu siasa.

Magufuli amesema hayo leo Jumanne, Septemba 15, 2020, wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kasharunga akiwa katika kampeni zake za kuwania urais ambapo ameingia mkoani Kagera.

“Miaka mitano iliyopita tulikuja kuomba kura hapa, Prof. Tibaijuka namfahamu tangu zamani, mumewe alikuwa Balozi Sweden mimi nikiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge mwaka 1995 nilikwenda huko, ndiyo maana alipogombea nilikuja nikawaomba mpeni Prof. Tibaijuka.

“Aliyekuwa Mbunge wa hapa (Masilingi) kabla ya Mama Tibaijuka alikuwa rafiki yangu, tumehangaika naye kwenye mabarabara, ndiyo maana alipomaliza muda wake nikamteua kuwa Balozi Marekani mpaka leo, ndiyo faida ya kuteua unayemfahamu.

“Palikuwa na diwani hapa alikuwa rafiki yangu, alikuwa akitusumbua sana, alikuwa wa chama kingine, nikasimama hapa akasema amehamia CCM leo ni Katibu wa CCM wa Wilaya, hata Mama Tibaijuka anasema amestaafu siasa lakini kwangu nasema hajastaafu.

“Huyu Dkt. Bashiru hakuna mtu alitegemea atakuwa Katibu Mkuu wa CCM Tanzania nzima, alikuwa muuza ndizi pale Kemondo, baadaye akaenda Chuo Kikuu Dar es Salaam na leo ndiyo Katibu Mkuu wa CCM Taifa.

“Mchakato wa kura za maoni ulipomalizika wa kwanza mpaka wa nne wote wametoka Nshamba, tulichambua tukasema:  Je, tumrudishe aliyekuwa wa kwanza, Katibu wa Prof. Tibaijuka anayelaumiwa hata nyumbani hajajenga nyumba? Tukamteua aliyejenga mpaka shule ya sekondari.

“Serikali hii ina vyeo vingi, Prof. Tibaijuka ameniambia mdogo wangu mimi nimestaafu, sasa nasema hujastaafu, hatuwezi kumuacha Profesa hivihivi kwa sababu kuna maeneo mengi ya kufanya kazi,”  amesema Dkt. Magufuli.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *